Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma
kuanzia Mei 13-18. Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah
Kibonde na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa.
Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah
Kibonde akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma
kuanzia Mei 13-18. na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa.
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imeandaa Maonyesho ya Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambayo yanatarajiwa kufanyika Mei 13 hadi 18 mjini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, alisema, makampuni na mashirika mbalimbali yanatarajia kushiriki wiki, ambayo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema
kuwa, maonyesho hayo itakuwa ni pamoja na mifuko shiriki kutoa elimu
kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, juu ya huduma ambazo
zinapatikana na tija yake katika taifa.
Aidha,
Irene aliongeza kuwa, SSRA inawataka wanachama wa PSPF kuondoa hofu juu
kutokuwepo kwa mafao yao katika mfuko huo, na kwamba mafao yao yako
salama na hakuna kitakachopoteza mafao ya wanachama hao.
Alisema kuwa, mfuko wa
PSPF utakuwa ukipewa bilioni 50 kila mwaka kwa ajili ya kwa ajili kuendelea
kufanya kazi zake kama kawaida .
Irene
pia, aliwataka wanachama wa mifuko mbalimbali kuwasilisha michango yao
kwa wakati ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifuko
kutokana na SSRA kutoa miongozo juu ya uendeshaji wa mifuko hiyo.
Alibainisha kuwa, mifuko yote imepewa miongozo katika
uendelezaji huduma wanazozitoa ikiwamo ya mafao kwa wafanyakazi wanaostaafu.
Alisema
kuwa tatizo lililokuwepo kwa mifuko ya PPF na NSSF, kujitoa kwa wingi
kwa wanachama wake, jambo linalochangiwa na waajiri, hali ambayo SSRA
inataka kuwafuatilia waajiri wanaowanyima wafanyakazi
haki zao.
No comments :
Post a Comment