Mwanamke - anayejiita Sister Phylis
Wanjiru Kamau, raia wa Kitui nchini Kenya akiwa ofisi za kamanda wa
jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, baada ya kukamatwa.
Taarifa za kipolisi, za kukamatwa kwa Sister Feki Phylis Wanjiru Kamau.
.....................................................................................
MAANDIKO
matatatifu ya kibiblia yanasema kuwa siku za mwisho yatatokea mambo
mengi ya kushangaza dunia ,kamwe kama dalili za siku za mwisho basi
naweza kusema ndizo hizi kwani kila kukicha ni mambo mapya ya
kushangaza .
Wakati
Taifa likiwa katika maswali yasiyo na majibu juu ya tukio la bomu
kuua Kanisani mkoani Arusha ,mkoani Iringa mwanamke mmoja
anayetambulika kwa Phylis Wanjiru ( 44)raia wa Kitui nchini Kenya amekamatwa akitaka kuwatapeli Masister wenzake .
Mwanamke huyo akiwa amevalia ya kitawa mfano
wa masister wa kanisa Kathoriki alikamatwa na kufanyiwa upekuzi
na kukutwa na baadhi ya vielelezo vilivyothibitisha utapeli wake
huo .
Wanjiru
ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya
masister wenzie kubaini kama si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya
baadhi ya masuala ambayo ni msingi wa utawa wao.
Taarifa
kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa zinaeleza kuwa
mwanamke huyo kabila lake ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika
nyumba za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.
Hata
hivyo mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya
ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip
(Line) za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.
Sister huyo feki alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.
Amesema
Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya
Rwanda, Uganda pamoja na nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni
alikuwa Mkoani Mara Tarime.
Sister huyo amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.
Sister huyo amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.
zaidi tembelea http://www.matukiodaima.com/
No comments :
Post a Comment