Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, March 31, 2012

WANANCHI WA ZILIZOKUA KOTA ZA BANDARI GEREZANI WAMEVAMIWA NA KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO KINYUME NA SHERIA


Wakili wa waliokuwa wenye nyumba zilizokua kota za Bandari na Trc, DKT. Sengondo Mvuni akizungumza na wateja wake leo na kusema kua mahakama iliungana na Serikali kuwahujumu Wananchi hawo
Wakili wa waliokuwa wenye nyumba zilizokua kota za Bandari na Trc, DKT. Sengondo Mvuni akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuhusu kufungua kesi ileile mahakamani
Baadhi ya wakazi waliokuwa kota za Bandari Gerezani wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa mkutano wao leo
Mwenyekiti wa wakazi wa Kota za Bandari Bi Fatma Msindi akizungumza kwenye mkutano huo leo
Mwenekiti akiongea Bi, Fatma Msindi
Wakili wa waliokuwa wenye nyumba zilizokua kota za Bandari na Trc, DKT. Sengondo Mvuni akizungumza na wateja wake leo na kusema kua mahakama iliungana na Serikali kuwahujumu Wananchi hawo


wananchi wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa kuusu kesi yao ya msingi leo
Wakili wa waliokuwa wenye nyumba zilizokua kota za Bandari na Trc, DKT. Sengondo Mvuni akizungumza na wateja wake leo na kusema kua mahakama iliungana na Serikali kuwahujumu Wananchi hawo

TAASISI YA HASSAN MAAJAR TRUST YAANZISHA DUKA LA HISANI MIKOCHENIMjumbe wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Zuhura Sinare Murro akizungumza katika uzinduzi wa duka la hisani la taasisi ya Hassan Maajar Trust uliofanyika kwenye jengo la Arcade Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo duka hilo linauza vifaa mbalimbali zikiwemo ngua za kiume, nguo za kike, viatu N.K.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Zena Maajar Tenga akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika asubuhi hii Mikocheni jijini Dar es salaam.
Wageni mbalimbali wakipata kifungua kinywa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa katika uzinduzi huo wakibadilishana mawazo.
Watoto kutoka shule ya msingi ya Ushindi Mikocheni wakiimba wimbo wa taifa katika hafla hiyo.
Mjumbe wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Zuhura Sinare Murro, katikati ni Mgoyela.
Mjumbe wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Zuhura Sinare Murro akionyesha ngua zilizopo katika duka hilo.
Wageni waalikwa wakiangalia nguo katika duka hilo.
Mdau Fredrick Njoka akiangalia suti katika duka hilo.

MKUTANO WA TAASISI ZA AFRIKA ZA UTAWALA BORA (AOMA) KANDA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAMWaziri wa Katiba na sheria Celina Kombani akifungua mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili unaowashirikisha wajumbe kutoka nchi za Ethiopia,Sudan ,Djibouti, Uganda, Afrika Kusini,Kenya, Tanzania na Burundi pamoja na mambo mengine unajadili masuala mbalimbali yatakayoweza kuboresha utendaji kazi wa nchi husika katika kuheshimu utawala bora na kulinda haki za binadamu.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
Rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (kulia) akizungumza na washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani
Washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kutoka nchi 9 za kanda ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka Tanzania Jaji kiongozi mstaafu Amir Manento (aliyesimama) wakati wa mkutano huo ambaye amewataka washiriki hao kubadilishana uzoefu na kuboresha utendaji kazi wa nchi husika katika kuheshimu utawala bora na kulinda haki za binadamu.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani (kushoto) akizungumza jambo na Rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (kulia) mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili unaowashirikisha wajumbe kutoka nchi 9 za Afrika leo jijini Dar es salaam. Katikati ni mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora nchini Tanzania Jaji kiongozi mstaafu Amir Manento.
Washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kutoka nchi 9 za kanda ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba (katikati mstari wa mbele), rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (wa pili kutoka kulia) na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania Jaji Ramadhani Manento (wa pili kutoka kushoto).

Nathan Mpangala wa Gazeti la Majira Ashinda Tuzo Ya Mchora Katuni Bora(EJAT)
.Nathan Mpangala Kwa wiki kadhaa sasa yuko mafunzoni nchini Mexico, akihudhuria kozi fupi ya waandishi wa habari, inayohusu Civil Resistance and Non violence Conflict. Hapa akiwa na baadhi ya washiriki wenzake toka sehemu mbalimbali duniani, wakiandaa michoro kwa ajili ya video itakayotumika kwenye kampeni ya familia zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na mauaji ya kila siku yanayohusishwa na biashara ya dawa za kulevya.
Nathan Mpangala pia usiku huu ameshinda tuzo ya wachoraji bora wa katuni katika tuzo za (AJET) zilizoandaliwa na Baraza la Habari (MCT) zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Hapa wakiendelea na kazi yao ya kuandaa katuzi hizo zinazohusu mauaji yanayotokana na madawa ya kulevya nchini Mexico.

Tuzo Za Wanahabari Bora
Rais Dk. Jakaya Rais wa T-anzania Jakaya Kikwete akiwa amewasili ukumbini tayari kwa kukabidhi tuzo hizo za waandishi Ijumaa usiku hapa katika picha akionekana kufuatilia ngoma ya asili kutoka kundi la Simba Theatre la jijini Dar es salaam. kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la habari Tanzania (MCT) Chande Omar na katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga nao wakifuatilia burudani hiyo.


Leo ndiyo leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo kunafanyika hafla kubwa ya utoaji wa tuzo ya Umahili wa uandishi wa habari kwa mwaka wa 2012 zinazoandaliwa na Baraza la Habari MCT na washirika wake ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Kikwete.

Wamejitokeza wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wasomi na waandishi wa habari wakongwe kama picha ya kwanza inavyoonekana kutoka kulia ni Profesa Aisha Yahya Othman mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Jenrrali Ulimwengu, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliyesimama na Profesa Shivji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika hafla hiyo usiku huu.


Hawa ni miongoni mwa majaji kulia ni Itillio Tagalile, Afisa Uhusiano wa Tanesco Badra Masoud na Wenceslaus Mushi wakijadili jambo.


Kushoto ni Awaichi Mawala kutoka Zantel na Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT Haika Mawala


Wageni waalikwa kutoka mashirika mbalimbali nao wamehudhuria katika hafla hiyo.


Majaji wakiwa katika meza yao.


Mwenyekiti wa bodi ya TANAPA Modestus Lilungulu kushoto na mjiumbe wa bodi Dk.Marcelina Chijoriga kulia wakiwa katika hafla hiyo.


Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Katibu mtendaji wa Baraza la Habari MCT Kajubi Mukajanga.


Mhariri kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo Jaquiline Liana akizungumza na Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo Juma Pinto kulia.


Clement Mshana Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji TBC akizungumza na Profesa Helmasi Mwansoko Mkurugenzi wa Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


Wadau kutoka Shelutete kutoka TANAPA na Geofrey Tengeneza kutoka TTB nao wapo katika hafla hiyo.Wanaharakati kutoka taasisi mbalimbali nao wamejongea katika hafla hiyo.


Kutoka kulia ni Mbunge wa Kondoa Kusini akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya bia ya Serengeti Graham Anderws


Bendi ya Msondo ikitumnuiza katika hafla hiyo.


Mzee wa Kammbi popote Antonio Lugas akiwa na mdau Abel Onesmo kutoka Clouds FM(picha zote na FullShangwe )

Katibu wa jukwaa la wahariri Tanzania Nevelin Meena aula tuzo ya habari za utawala bora ,gazeti la Uhuru latoa mpiga picha bora , majira mchora katuni bora , ITV yachukua tuzo ya habari utawala bora upande wa radio Noel Thomson aula, wateule wa magazeti habari za Maralia ni gazeti la Rai ,upande wa radio katika Maralia ni TBC ,upande wa magazeti ni IMani Imani .

Tuzo za michezo ni radio ni Abdala Machura kwa upande wa TV KIbanda amtabiria Bw.Annual Mkama afuta matokeo

Upande wa magazeti ni David Azaria wa gazeti la Habari leo kaibuka Mshindi wa habari za walemavu upande wa TV ni Lekoko Livilala upande wa Radio ni walioshindana ni Mliamani Radio na TBC one Tuma Dandi aibuka kidedea kutetea walemavu wenzake ,Nasra Abdala Kutoka gazeti la Tanzania Daima kashinda tuzo ya habari ya jinsia

Tuzo habari ZA UKIMWI katika magazeti imechuliwa na Elias Msuya kutoka gazeti la Mwananchi ,katika radio ni Betrice Nangawe kutoka radio Sun ,upande wa tuzo ya afya upande wa magazeti tuzo imekwenda kwa Sharifa Kalokola kwa upande wa radio ni Secelia Ndamakigezi ,tuzo ya mazingira kwa upande wa magazeti imechukuliwa na Lukas Liganga tuzo ya habari uchumi na biashara imekwenda kwa Bw Mashira upande wa TV ni zawadi imekwenda TBC kwa kuchukuliwa na Aneth Andwer .

Tuzo ya habari za Elimu kwa magazeti kwa Erick Kabembera upande wa TV imekwenda kwa TBC Dodoma kwa Bi. Victoria Patrick kwa upande wa radio tuzo imekwenda kwa Grece Kihondo ,tuzo ya habari wa watoto katika magazeti imekwenda kwa Nashon Kenedy ,upande wa TV ni Anganile Mwakanjala wa TBC amekuwa pekee.
Upande wa Radio tuzo ya watoto imekwenda kwa Sempaka Mchome

Tuzo ya hifadhi ZA Taifa katika magazeti imekwenda kwa Paul Jems kwa upande wa Radio imekwenda kwa TBC Taifa kwa Alex Magwesa ,huku tuzo ya utalii wa ndani upande wa magazeti imekwenda kwa Monica LUhondo awapiku Kalulunga na Midelo ,upande wa TV ni Juma Lugasi upande wa radio hakuna mshindi.

Tuzo ya maafa na migogoro katika magazeti ni Daniel Mbega ,katika TV ni Joseph Bula ambaye habari zake mbili zote ziliingia katika shindano hilo tuzo ya sayansi na Teknolojia imekwenda kwa Benard Lugongo kwa upande wa gazeti na radio ni Abel Mwende wa Claus Fm akosa mpinzani na kwa magazeti ni Nevelin Meena kwa TV hakuna Mshindi .

Tuzo ya habari zanye mvuto kwa watu upande wa magazeti ni P. Machira kwa upande wa habari za michezo na burudani upande wa TV ni Anual Mkama wa Mlimani TV akosa mpinzani ,

Kwa upande wa washindi wa jumla tuzo imechukuliwa na Nevelin Meena wa Mwananchi akabidhiwa tuzo na Rais Jakaya Kikwete aibuka na kitita cha kufa mtu dola kasha za kujiendeleza Masomo zatolewa kwake .wakati tuzo ya maisha ya mafanikio katika maisha katika tasinia ya habari imechukuliwa na Philip Karashan aliyejipatia shilingi milioni 10

Friday, March 30, 2012

KAMPUNI YA TIGO YAFUNGUA OFISI YA HUDUMA KWA WATEJA BAADA YA MATENGENEZO MAKUBWA MLIMANI CITY

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt, Cyril Chami akiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya tigo baada ya kuzindua ofisi
ya huduma kwa wateja baada ya matengenezo makubwa mlimani city leo

Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akipatiwa maelezo ya moja ya bidhaa za
simu zilizopo

simu
humeiona muheshimiwa
Waziri wa viwanda na biashara Dkt.Cyril Chami akikata
utepe kuashiria uzinduzi huo leo kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Tigo Bi.Hilda Damas
Msema Chochote Sauda Simba Kilumanga akionea

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo waliokuwepo katika ufunguzi huo
wakiwa katika picha ya pamoja leo

Tuesday, March 27, 2012

TOMASI MASHARI AJIFUA KUMKABILI SELEMANI GALILE APRIL 9


Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kulia akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Tomasi Mashari akifanya Mazoezi leo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Selemani Galile litakalofanyika April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)