Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 16, 2012

KAJALA KIZIMBANI

MSANII wa filamu
nchini Kajala Masanja na mumewe
Faraja Chambo wamefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa
na mashtaka matatu likiwemo la kula njama,
kuhamisha umiliki wa nyumba na
kutakatisha fedha haramu. Akisoma hati ya
mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi,
Sundi Fimbo, Mwendesha Mashtaka wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Leonard Swai alidai kuwa
mwaka 2010 , Kajala na Chambo walikula
njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba
iliyopo Kunduchi Salasala wilaya ya
Kinondoni kinyume na kifungu cha 34 cha
sheria ya rushwa ya mwaka 2007 sura ya
11. Swai alidai kuwa Aprili 14, 2010
jijini Dar es Salaam washtakiwa hao kwa
pamoja kinyume na kifungu cha 34
(2)a(3) cha sheria ya kuzuia na kupambana na
rushwa walihamisha umiliki wa
nyumba hiyo iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar
es Salaam. Alidai kuwa siku
hiyo ya Aprili 14,2010 washtakiwa hao ambao ni mtu
na mkewe walifanya
uhamisho wa umiliki wa nyumba hiyo iliyopo Kunduchi Salasala
ambayo
ilipatikana kutokana na fedha haramu. Wakati kesi hiyo ikiendelea
Kajala
pekee ndiyo aliyokuwepo mahakamani hapo na mumewe Chambo ambaye
anakabiliwa na
kesi nyingine za kutakatisha fedha haramu mahakamani hapo
hakuwepo. Katika kesi
hiyo, Kajala anatetewa na Wakili Alex Mgongolwa ambaye
alidai mahakamani hapo
kuwa Wakili huyo wa Takukuru , Swai hana mamlaka ya
kusikiliza kesi hiyo na
kwamba hati ya mashtaka inamapungufu. Akijibu hoja:
Wakili Swai alidai kuwa
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliteua mawakili wa
Takukuru chini ya Government
Notice (GN) 168 ya mwaka 2010 na kuwaruhusu
kuendesha kesi zisizokuwa za rushwa
na kwamba katika uteuzi huo yeye alikuwa
ni mmojawapo. Hivyo anauhalali wa
kuendelea kuendesha kesi hiyo. Hakimu Fimbo
ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili
20, mwaka huu atakapotoa uamuzi juu ya
hoja hizo.
HABARI KWA
HISANI YA MWANANCHI

No comments :

Post a Comment