Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani akifungua mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili unaowashirikisha wajumbe kutoka nchi za Ethiopia,Sudan ,Djibouti, Uganda, Afrika Kusini,Kenya, Tanzania na Burundi pamoja na mambo mengine unajadili masuala mbalimbali yatakayoweza kuboresha utendaji kazi wa nchi husika katika kuheshimu utawala bora na kulinda haki za binadamu.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
Rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (kulia) akizungumza na washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani
Washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kutoka nchi 9 za kanda ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka Tanzania Jaji kiongozi mstaafu Amir Manento (aliyesimama) wakati wa mkutano huo ambaye amewataka washiriki hao kubadilishana uzoefu na kuboresha utendaji kazi wa nchi husika katika kuheshimu utawala bora na kulinda haki za binadamu.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani (kushoto) akizungumza jambo na Rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (kulia) mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili unaowashirikisha wajumbe kutoka nchi 9 za Afrika leo jijini Dar es salaam. Katikati ni mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora nchini Tanzania Jaji kiongozi mstaafu Amir Manento.
Washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kutoka nchi 9 za kanda ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba (katikati mstari wa mbele), rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (wa pili kutoka kulia) na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania Jaji Ramadhani Manento (wa pili kutoka kushoto).
No comments :
Post a Comment