Adam Kighoma Malima |
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Adamu Kighoma Malima amekombwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh.
milioni 15 katika hoteli ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro.
Taarifa za kipolisi
zilizopatikana kutoka mjini Morogoro zimethibitisha kutokea wizi huo zikisema
ulitokea usiku wa kuamkia leo.
Zilimkariri Mkuu wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, Hamis Seleman taarifa zilmesema wizi umetokea
wakati waziri huyo alipokuwa amejipumzisha kwenye sebule ya chumba chake kwenye
hoteli hiyo hadi mida ya 10.45 ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi
chumbani.
Kwa mujibu wa polisi zimeibwa
fedha taslimu Dola 4000 za Marekani na Sh. milioni 1.5, pete mbili za silva
zenye thamani ya sh. milioni 2, simu zenye thamani ya sh. milioni 1.3,
balaghashia yenye thamani ya sh. 50,000, laptop mbili zenye thamani ya sh.
milioni 5.6, taperecorder na headphone vyote vya sh. milioni moja.
Polisi wanasema dirisha la
aluminium la chumba cha hoteli alimokuwa Malima limekutwa limevunjwa kwa kitu
kigumu.
Habari zinasema nje ya dirisha
hilo zimeoneka nyayo nje na ndani ya chumba jambo linaloashiria kuwa ni za
mwizi.
Kufuatia wizi huo, walinzi watatu
wa hotel hiyo wanashikiliwa na polisi huku taarufa zilizopatikana baadaye
tukiandaa kurusha ripoti hii zikisema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa
vimepatikana, ingawa havikutajwa.
No comments :
Post a Comment