CHAMA
CHA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI CHATAMBULIKA
KIMAT AIFA
Na
Mwandishi
Wetu
SHIRIKISHO la Dunia la ngumi za kulipwa (WPBF) limempa
hati ya kuwa
mwakilishi wa Shirikisho hilo nchini Rais wa Shirikisho la ngumi
za kulipwa
nchini (TPBO).
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kwa
mtandao na Rais
wa TPBO Yassin Abdala 'Ustadhi' ilisema kuwa Shirikisho hilo
lenye makazi yake
nchini Marekani limempa hati hiyo ambayo itamruhusu kutoa
taarifa muhimu za
jinsi mabondia wa ngumi za kulipwa wa Tanzania
wanavyoingizwa katika viwango vya
Shirikisho hilo.
Alisema, sambamba na
hilo pia litawasaidia mabondia
watanzania kuweza kupata nafasi ya kugombea
mikanda ya Shirikisho hilo.
"Ni
jambo zuri kwa mabondia watanzania kwani
watakuwa wanajua kila kitu kuhusu
viwango vyao kuingizwa katika Shirikisho
hilo lakini pia kupata nafasi ya
kuwania mikanda hiyo ambayo itamsaidi
kutambulika Ulimwenguni,"
alisema.
Sambamba na hilo pia Ustadhi
amempongeza Mpiga picha wa Kampuni ya
Business Times Limited inayochapisha
magazeti ya Majira, Spoti Starehe na
Business time,pamoja na Jarida la
Maisha, ambaye pia ni Kocha wa Kimataifa wa
Mchezo wa Masumbwi, Rajabu
Mhamila 'Super D' kwa mchango wake katika kuhakikisha
anaukuza mchezo wa
ngumi bila kubagua.
Alisema, Super D amekuwa ni msaada
mkubwa sana katika
kila maandalizi ya mchezo kwa kuwasaidia waandaaji ambao
hupungukwa vifaa
vinavyohusu mchezo hususan glovus na vifaa vingine.
Sambamba
na hilo
amekuwa akifuatilia mapambano ya ngumi popote pale hata mkoani ,na
huku
akiyaripoti yote yanayofanyika huko nje ya Dar es salaam kwa galama
zake
mwenyewe.
"TPBO tunayo macho yenye kuona na kuthamini michango ya
watu wa
aina yako hivyo tunakuahidi kukupatia cheti cha kuthamini mchango
wako katika
tasnia hii ya mchezo wa ngumi katika wakati muafaka,"
alisema.
Aliongeza
kuwa yapo mengi ya kumshukuru kwani pia ameakuwa
akiwasaidia mabondia wa mikoani
kwa kuwauzia vifaa vya mchezo kwa bei ndogo
kuliko hata ile ya madukani , hivyo
kuwawezesha mabondia hao kuwa na uwezo wa
kumiliki vifaa vya ngumi kiurahisi

No comments :
Post a Comment