Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, March 15, 2012

AIRTEL YAJA NA INTERNET YA 3.75G YENYE KASI NA UBORA ZAIDI

Mkurugenzi Mkuu wa
Airtel, Sam Elangalloor akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Airtel 3.75G hii
leo jijini Dar es Salaa katika makao makuu ya Kampuni hiyo.
Beatrice Singano
Mallya ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasilianowa Airtel akizungumza wakati wa
uzinduzi huo hii leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Sam Elangalloor.
Mambo ya airtel
internet 3.75G
Waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia uzinduzi
huo!
Meneja Uhusiano wa
Airtel Tanzania Jackson Mmbando akielezea machache juu ya huduma yao
mpya.
Meneja Maendeleo wa
Bidhaa wa Airtel, Salum Madati akifafanua juu ya bidhaa hiyo mpya iliyozinduliwa
hii leo.
---
Airtel Tanzania leo
imepiga hatua kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G
Africa kwa kuzindua rasmi mtambo wa 3.75G nchini Tanzania,ambapo Airtel itatoa
huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi kwa watumiaji wenye simu zenye
uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote.

Mkurungenzi Mkuu wa
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangalloor alieleza” kukua kwa
technolojia hii kutakuza ufanisi katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano
(multimedia), kwa kuwa 3.75G itatoa internet yenye ubora na kasi zaidi kwa
kuwezesha wateja kufungua tovuti mbalimbali, kufanya maongezi ya simu kwa njia
ya video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia kupata muziki
kutoka kwenye tovuti kwa kutumia simu.

Teknologia ya 3.75G
itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya data kwa njia tofauti na ya pekee
kabisa, ndio maana leo Airtel tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni
uvumbuzi na muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa
Airtel wote nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya juu
pamoja na kasi zaidi”

Tunafanya ubunifu
wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao kwa kuzingatia kuwa sasaivi
dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za kimtandao hasa kupitia simu ya
mkononi
Ukirejea takwimu
zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co. Telecommunications zinaonyesha
mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na
kwamba bara la Afrika ni moja kati ya soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko
la simu za mkononi likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma
za internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking) na biashara kwa njia
ya mtandao yaani (mobile commerce) .

Hivyo basi kwa
kuzingatia hili, ndio maana Airtel tunaendelea na mikakati kama hii ya kuwaletea
wateja internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ambayo ni sambamba na lengo letu la
kuendea kupanua mtandao ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi
wa vijijini ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara
la Afrika.

“wote tunafahamu
kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii ya sasa lakini bado
kunachangamoto kubwa sana katika kupata huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani
Africa.

Lakini tukumbuke
Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa kupitia
mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini tutaweza
kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani na nje ya ya jamii
zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu, pamoja na kupanua wigo wa wale
wanaofanya biashara kupitia mtandao wa internet “ Aliongeza
Elangalloor.

Ikiwa tayari mteja
ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or
HSPA. Hii inategemeana na Aina ya simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya
kuunganishwa ni yenye ubora zaidi.

Airtel itaendelea
kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote huku lengo likiwa ni kuwa
mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G katika bara zima, na itaendelea kutoa
huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watumiaji.

No comments :

Post a Comment