Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 9, 2012

MATUMLA ATAKIWA MAANDALIZI MEMA NA WANAFUNZI WA ARUSHA

WANAFUNZI
WA SHULE ZA MOSHI WAMWANDIKIA
BARUA RASHID MATUMLA!!

Wanafunzi wanne wanaosoma katika shule za msingi
na
sekondari za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wamemwandikia barua bondia Rashid “Snake Man” Matumla wakimtakia kila la kheri katika mpambano
wake
na Vitaly “Siberia Tiger” Shemetov wa Urusi. Wanafunzi hao
Levina
Joachim(Shule ya Msingi Mwereni), John Makupa (Mawenzi
Secondary),
Ashura Omari (J.K Nyerere Secondary) na Oliva Philip (Shule ya
Msingi ya
Majengo) wamemwelezea Rashid “Snake Man” Matumla kama
tegemeo kubwa la
Taifa. Ifuatayo ni baadhi ya sehemu za barua zao:

“Mpendwa Golden Man, kama katika riwaya ya
Sinderela
natamani ungekuwa Prince wangu ninayekungojea unichukue katika
mikono yako”
alisema Ashura Omari katika barua yake. “Nakutakia ushindi
mnono ili utimize ndoto zangu za wewe kuwa shujaa
wangu kwa kumwonyesha Tiger
huyo wa Siberia kuwa Tanzania tuna mabingwa wa
kweli”
Ashura Omari
alimalizia katika barua yeke.
Oliva
Philip
alisema “Ni muda mrefu mji wa Moshi haujaweza kushughudia
burudani kama
utakayoileta wewe hivi karibuni. Naamini kuwa utaendelea
kuungarisha mji wa
Moshi ili kweli ujulikane kuwa ni kilele cha
Afrika”
Naye
Levina
Joachim alisema “Golden man wewe ni nuru ambayo Tanzania iliipoteza kwa muda mrefu na tunakutegemea kuwa utairudisha
na
kuifanya ingare kila siku, nakutakia ushindi mzuri”
John Makupa
alisema
“Ningekuwa na uwezo ningekuja ulingoni siku hiyo nikakusaidia
kushika mguu mmoja
wa Tiger huyo wa Siberia ili umchakaze vizuri, lakini
naamini kuwa utamuonyesha
kuwa kweli wewe ni moto wa kuotea
mbali”
alisema Makupa.
Mpambano wa
ngumi
kati ya Rashid “Snake Man” Matumla na Vitaly “Siberian Tiger”
Shemetov
wa Urusi umeanza kuwa ni gumzo kubwa katika Manispaa ya Moshi huku
wenyeji
wengi wakifurahia na kungojea kwa matumaini makubwa ushindi wa
Matumla siku ya
tarehe 22 Juni mwezi wa sita.
Mpambano
huo
ambao utakuwa ni wa TPBC International Title katika uzito
wa Super Middleweight utawakutanisha miamba miwili ya ngumi
duniani.
Mgeni mashuhuri katika mpambano huo atakuwa mcheza sinema mashuhuri
wa Marekani Deidre Lorenz toka katika jiji la New York.
Hii
itakuwa
mara ya kwanza kwa mpambano wa ngumi hapa Tanzania na Afrika nzima
kuhudhuriwa
na mcheza sinema mashuhuri kutoka Hollywood, nchini Marekani
hivyo kulipa
pambano hili sura mpya kabisa.
Bibi
Deidre
Lorenz atakuwa njini Moshi kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 17 Juni na
pia
kushiriki katika mbio za 22 za Marie Frances Mount Kilimanjaro
Marathon

ambazo zimepewa hadhi ya kuwa “Mbio za Marathon za kumbukumbu
ya miaka 50 ya
Uhuru wa Tanganyika
” na Bodi ya Utalii ya Tanzania
(TTB).
Mpambano
huu
una promotiwa na kampuni ya ASMM Peak Gemstone Traders LTD ya
mjini Moshi
na utajumuisha pia mabondia kadhaa kwenye mapambano ya
utangulizi:
Pascal
“Prince Kilimanjaro” Bruno
atapambana na James “Sura Mbaya” Kitasi wa
Kenya katika uzito wa Light Middle
raundi 10 ubingwa wa Afrika ya
Mashariki
. Bruno atakuwa anatetea
mkanda wake wa ubingwa wa Afrika ya
Mashariki.
Naye Alibaba “Dragon” Ramadhani atatetea mkanda wake wa Afrika
ya
Mashariki
akichuana na Sebyala Med toka nchini Uganda katika
uzito wa
Middle

No comments :

Post a Comment