Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 16, 2012

MWIGIZAJI WA FILAMU KAJALA MASANJA APANDISHWA KIZIMBANI

Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu
yakiwamo ya kutakatisha fedha haramu kosa ambalo halina dhamana kisheria na
hivyo kurudishwa lupango.
Katika kesi hiyo, Kajala anashitakiwa
pamoja na mumewe Faraji Mchambo ambapo makosa mengine ni kula njama na
kubadilisha umiliki wa nyumba.
Wakili wa serikali Leonard Shayo
mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alidai kuwa Kajala na mumewe wameshitakiwa kwa
kosa la kwanza la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote walitenda kosa hilo la
kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es
Salaam.
Shtaka la pili walidaiwa kuwa mnamo Aprili 14 2010
walihamisha umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Ambapo shtaka la
tatu walidaiwa Aprili 14 2010 huku wakijua ni kinyume na sheria walifanya kosa
la kutakatisha fedha haram ambapo ni kosa lisilo na dhamana kisheria
.
Chambo hakuwepo mahakamani kwasababu yupo gerezani mahabusu kwa
makosa mengine ambayo hayana dhamana yanayomkabili ya utakatishaji
fedha.
Kajala alikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kwa
uchungu mkubwa huku akilia pamoja na ndugu zake akiwamo mama yake aliyekuwepo
mahakamani hapo.
hakimu Fimbo aliahirisha kesi hiyo mpaka Aprili 20
mwaka huu ili kesi ije kwaajili ya kutajwa na pia kutolea maamuzi,maombi
yaliyotolewa na wakili wa Alex Mgongolwa anayemtetea kajala kwa habari zaidi
tembelea full shangwe

No comments :

Post a Comment