Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, March 17, 2012

THABEET KATIKA TIMU YA TATU NBA

THABEET
KATIKA TIMU YA TATU NBA


Hasheem Thabeet katikati na
jezi
ya timu yake mpya
MCHEZAJI wa kulipwa wa mpira wa kikapu wa Tanzania,
Hasheem
Thabeet amechukuliwa
na klabu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki kwenye
Ligi
ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kutoka klabu ya Houston
Rockets.
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mitandao mbalimbali
ya
intaneti, Portland Trail Blazers imefanikiwa kumnyakua Mtanzania huyo
kutoka
Rockets kwa kubadilishana na mchezaji mwingine Marcus Camby, jana
ambayo ilikuwa
siku ya mwisho iliyowekwa na NBA kwa ajili ya
klabu zinazocheza ligi hiyo kufanya utaratibu huo
wa
kubadilishana wachezaji.
Mlinzi Jonny Flynn, pia amejiunga na klabu ya
Portland
Trail Blazers kama sehemu ya utaratibu huo, Thabeet ambaye sasa
amechukuliwa na
Blazers kabla alichukuliwa na Houston Februari mwaka jana,
akitokea Memphis na
alifanikiwa kuichezea Rockets mechi tano pekee
katika msimu huu wa ligi.
“Tunatazamia kuwa yale yatakayofanywa na Jonny pamoja
na
Thabeet yanaweza kuleta mafanikio katika timu yetu na pia tunamshukuru
Marcus
kwa mchango alioutoa kwa kipindi cha misimu mitatu aliyokuwa nasi na
tunamtakia
kila la heri huko alikoenda,” alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Blazers
Chad
Buchanan.
Katika michezo 120 ya misimu mitatu akiwa na klabu
za
Memphis na Houston, Thabeet mwenye umri wa miaka 25, ana wastani wa pointi
2.2,
na jumla ya dakika 10.7 pamoja na rebaundi 2.

No comments :

Post a Comment