Kumwelimisha mwanamke ni
kuielimisha jamii nzima Airtel Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania
kupitia kitengo cha huduma Kwa jamii imezindua programu ya uwezeshaji kwa
wasichana itakayo wawezesha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 18
katika harakati za kufanikisha malengo yao ya baadae na kuwajengea uwezo wa
kujiamini huku mafunzo hayo yakiwa yamebeba ujembe usemao “jenga maisha yako ya
baadae”
kuielimisha jamii nzima Airtel Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania
kupitia kitengo cha huduma Kwa jamii imezindua programu ya uwezeshaji kwa
wasichana itakayo wawezesha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 18
katika harakati za kufanikisha malengo yao ya baadae na kuwajengea uwezo wa
kujiamini huku mafunzo hayo yakiwa yamebeba ujembe usemao “jenga maisha yako ya
baadae”
Akiongea wakati wa
ufunguzi wa Programu hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana Canossa
iliyopo Tegeta jijini Dar-es-Salaam Meneja Huduma kwa jamii Bi Tunu Kavishe
alisema “Programu yetu ina lenga kuwawezesha wasichana wote walioko shule za
sekondari ikiwa ni muendelezo wa dhamira ‘Airtel Shule yetu’ ya kutoa elimu kwa
jamii hasa wasichana ili kuendeleza mahusiano yetu mazuri kati ya kampuni na
wateja wetu waaaminifu.
Mbali na hayo ni ukweli
kwamba wasichana wanahitaji sana uelewa wa kutosha pamoja na kutimiza malengo
ili kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa au katika ramani ya dunia, Airtel
inaamini wasichana hawa wanahitaji nafasi zaidi, mbali na masomo wanayosoma
wanatakiwa kujifunza mbinu mpya za maendeleo kutoka kwa wasichana wenzao na
wakubwa ambao wamewazidi umri pia.
Nae,Mkurugenzi wa huduma
kwa wateja wa Kampuni ya Airtel Bi.Adriana Lyamba ambae ndie aliyekuwa mtoa mada
katika ufunguzi wa program hiyo kwa mara ya kwanza alisema “najisikia fahari
sana kwa Airtel kunipa nafasi ya kuwa mtoa mada wa kwanza mara baada ya ufunguzi
wa program
hii ya kuwawezesha wanawake wenzangu katika shule za sekondari ya
wasichana ya Canossa.
Naiomba Airtel
kuhakikisha programu hii itaendelea kwa shule nyingine za wasichana Tanzania na
igusie mitaala mbali mbali ya uendelezaji wa taaluma kwa wasichana kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika maisha.tutawaomba
wafanyakazi wengine wa
Airtel pamoja na wadau wetu katika biashara kujumuika
nasi ili kuwaongezea na kuwapa wanafunzi uzoefu na mbinu mbalimbali kwa kufanya
hivyo itawaweze kuelewa ni jinsi gani wataweza kuchagua na
kuendeleza
taaaluma bora kwa maisha yao”.
“Kuna
msemo unaosema kuwa ‘kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima’ kwahiyo
tunaamini elimu mtakayotoa sasa itakuwa chachu ya maendeleo kwa vizazi vijavyo”
aliongeza Bi Adriana Tumejidhatiti kuisaidia jamii ya kitanzania,mbali na
programu hii ya kuwawezesha wasichana tumekuwa tukisaidia sekta ya elimu kupitia
programu ya Shule Yetu kwa kugawa vitabu katika shule za sekondari nchini na nia
yetu ni kuendeleza kiwango cha elimu kwa kuwezesha upatikanaji wa vitabu kwa
urahisi zaidi kwa wanafunzai wa shule ya sekondari.tangu tulipoanza hii programu
ya kusadia vitabu katiaka shule ya sekondari kwa miaka saba iliyopita tumeweza
kuwafikia zaidi ya sekondari 800 ambazo zipo nchi nzima
No comments :
Post a Comment