Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 16, 2012

MILIONI 26 KWA YA KUCHANGIA MADAWATI KUPITIA TIGO TUCHANGE

Tigo Tuchange yachangia madawati ya shule
15
Machi, 2012, Dar es Salaam. Zaidi ya watu wapatao mia moja walishiriki katika
matembezi ya kujitolea katika ufunguzi wa kampeni ya Tigo Tuchange kwa ajili ya
kukusanya hela ya kuchangia sekta ya elimu nchini Tanzania. Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya ufundi, Mh. Shukuru Kawambwa alizindua matembezi hayo Machi 3, 2012,
kwa kukata utepe na kuwaongoza watembeaji kutoka Shekilango Millenium Bussiness
Complex hadi Ubungo mataa. Nchini kote, maelfu ya watu walijitokeza na kuongeza
muda wa maongezi kupitia Tigo Rusha ili kuchangia kampeni hii.
" Ningependa
kuwashukuru wote walioshiriki kuchangia kampeni ya mwaka huu" alisema Bw. Diego
Gutierrez, ambaye ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kampuni ya Tigo. " Tunafuraha
kufahamu kuwa matokeo ya juhudi zetu za pamoja zitaleta mabadiliko kwa mamia ya
watoto wa shule nchini" alisema.

Shiling milioni 26 zimekusanywa kupitia
muda wa maongezo ulionunuliwa kupitia Tigo Rusha Kati ya saa tano na saa sita
mchana wa siku hiyo. Wateja walionunua muda wa maongezi kati ya muda huo,
waliweza kutumia muda wao wa maongezi kama kawaida wakati Tigo ilirudufu kiasi
hicho na kuingiza katika kampeni hiyo ya uboreshaji wa Elimu. Fedha zote
zilizopatikana katika tukio hilo zitapelekwa kwa Hassan Majaar Trust (HTM),
programu endelevu yenye lengo la kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa
kutoa madawati kwa shule mbalimbali zenye uhitaji.
Mwenyekiti wa HTM, Balozi
Mwanaidi Maajar, alisema "Tumefarijika sana na kampeni hii na tungependa
kuwashukuru Tigo kwa mchango huu utakaosaidia mahitaji ya elimu kwa watoto wa
Tanzania. Msaada huu tulioupata leo utatumika katika kununulia madawati kwa
shule mbalimbali ambazo tunazo na tumethibitisha kuwa na uhitaji. Lengo letu ni
kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati. Tunaona kwamba hii ni
hatua kubwa katika kufikia malengo yetu".
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao
wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao
wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote
nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A
(MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana
maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13
yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.
Msingi wa mafanikio ya Tigo ni
uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji
.Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana
kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma
bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na
Zanzibar.
Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.tigo.co.tz/

No comments :

Post a Comment