Mabondia, Selemani Galile kushoto na Tomasi
Mashali wakitazamana kwa usongo wa
kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa
ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa
Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini
TPBO walipokuwa wakitambulisha mpambano
wao. Dar es Salaam jana,
utakaofanyika Apri 9.katikati ni Rais wa Oganaizesheni
hiyo Yasin Abdallah
Mwaipaya.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)
GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA MABONDIA Selemani
Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa
ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika
katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.Pambano hilo linatarajiwa
kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.Wakitambiana Dar es
Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha
anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika
atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao."Mkanda lazima niiuchukue kwani
najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini
na mkanda ni wangu," alisema Galile.Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi
10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi
ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa."Ninauwezo,
nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio
zitaamua nani bingwa," alisema.Naye kwa upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah
alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo
alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa
atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzaniMbali ya kuwepo na mpambano
huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi
wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled,David Haye, Waldmil
Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengiZitakuwa
zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na
kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo
wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa
mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi
nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing
Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi
Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.
No comments :
Post a Comment