Mheshimiwa
Waziri Shukuru Kawamba,
Wawakilishi
kutoka Hassan Maajar Trust,
Wafanyakazi
wa Tigo,
Ndugu
waandishi wa habari,
Mabibi
na mabwana,
Naomba
mniruhusu kuongea na nyie leo na kiswahili changu ambacho sio kizuri sana,
lakini kwenye hii siku maalum ningependa nijaribu
Nina
furaha kuwakaribisha wote katika siku hii nzuri ya kampeni ya Tigo Tuchange.
Tuna furaha kumkaribisha Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi, mheshimiwa Shukuru
Kawambwa kama mgeni rasmi.
Tigo
Tuchange ni moja ya sehemu yetu ya kusaidia jamii nchini Tanzania. Mchango wa
leo unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi katika shule zenye
upungufu wa vifaa, hivyo kuwawezesha kufanya vyema katika masomo yao.
Kati
ya saa tano asubuhi na saa sita mchana leo, muda wa maongezi utakaonunuliwa
kupitia Tigo Rusha,utaongezwa na Kampuni yetu,
kwa kiwango kile kile na fedha zote zitaingia moja kwa moja kwenye
kampeni.
Tulizindua
Tigo Tuchange mwaka jana,na tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kukusanya
kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano nukta tisa,ambazo zilitumika
kununua vitabu na vifaa vingine katika shule mbalimbali nchini. Mwaka huu
tunatarajia mafanikio zaidi. Hassan Maajar Trust ni moja kati ya watakaofaidika
na kampeni hii,vifaa vingine vya elimu vitatolewa ambavyo vitanufaisha
wanafunzi wa shule za msingi.
Asanteni, na kwa pamoja tufaye mabadiliko yatakayoboresha mazingira ya wanafunzi!
No comments :
Post a Comment