Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, March 10, 2012

WAZIRI AZINDUA AKAUNTI YA TWIGA STARS TIGO PESA

Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara leo (Machi 10 mwaka huu) amechangia
sh. milioni moja kwenye uzinduzi wa akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa
kuichangia timu hiyo ambayo inashiriki michuano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake
(AWC).
Akizungumza kwenye hafla hiyo
iliyofanyika Dar es Salaam, Dk. Mukangara alisema ni jukumu la kila Mtanzania
kuichangia Twiga badala ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuachiwa
pekee mzigo huo wa kuendesha timu hiyo.
Wachangiaji wa Twiga Stars
wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389 ambapo kiwango cha juu
kinachoweza kutumwa kwa muhamala (transaction) mmoja ni sh. 500,000. Kwa Waziri
Dk. Mukangara kuchangia sh. milioni moja alifanya mihamala miwili.
Naye Makamu wa Kwanza wa Rais wa
TFF, Athuman Nyamlani alisema Twiga Stars kwa sasa haina mdhamini na Shirikisho
limekuwa likibeba mzigo wa kuhakikisha inashiriki katika mechi za kirafiki na
mashindano mbalimbali kwa vile imekuwa ikifanya vizuri.
Twiga Stars inayofundishwa na
kocha Charles Boniface Mkwasa iko kwenye raundi ya pili ya mashindano ya Kombe
la Afrika kwa Wanawake (AWC) ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini
Addis Ababa.
Katika raundi ya kwanza, Twiga Stars iliitoa Namibia kwa
jumla ya mabao 7-2. Ilishinda ugenini 2-0 na kuibuka na ushindi mnono nyumbani
wa mabao 5-2. Fainali za AWC zitafanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial
Guinea.

No comments :

Post a Comment