Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 9, 2012

HABARI LUKUKI KUTOKA TFF


Release No. 035
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 9, 2012
UENDELEZAJI WA WAAMUZI WATOTO WA
TWALIPO
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na mpango wake wa kuwaendeleza waamuzi
watoto wa Kituo cha Kambi ya Twalipo kilichoko Mgulani jijini Dar es Salaam kwa
kuwapa mafunzo zaidi na kuwatumia katika mashindano mbalimbali.
Lengo ni
kuboresha uwezo wao katika kuchezesha mchezo wa mpira wa miguu na kutoa
changamoto kwa vijana wadogo wengine, hasa wa shule za msingi, sekondari na
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kuingia katika uamuzi ili kujenga kizazi
kipya katika fani hiyo.
Wazo la kuwa
na waamuzi watoto lilianzia kwa Meja Bakari wa kituo hicho, juhudi ambazo TFF
inazipongeza na kuziunga mkono kwa kutoa mafunzo zaidi kwa wahusika. Wiki mbili
zilizopita tuliwaandalia mafunzo zaidi ya kuwanoa ambayo yaliendeshwa na
Mkufunzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Leslie
Liunda.
TFF
imeshawatumia waamuzi hao watoto katika mashindano ya vijana wenye umri chini ya
miaka 20 (Kombe la Uhai), michuano ya vijana ya Rollingstone iliyofanyika jijini
Arusha na fainali za Copa Coca-Cola. Mashindano yote hayo yalifanyika mwaka jana
na kiwango walichoonesha waamuzi hao kilikuwa kizuri.
Hivyo
tutaendelea kuwapa mafunzo zaidi na mashindano mengine kadri tutakavyoona inafaa
kwa lengo la kuwajenga na kuwaongezea ujuzi.
SITA VPL
UWANJANI WIKIENDI
Michuano ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi
hii kwa mechi tatu zitakazokutanisha timu sita kwenye viwanja
tofauti.
Yanga itakuwa
mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa kesho (Machi 10 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam. Machi 11 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Simba na Toto
Africans ya Mwanza itakayochezwa kwenye uwanja huo huo.
Viingilio
katika mechi hizo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh.
5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa viti vya VIP C na B wakati
VIP A itakuwa sh. 15,000.
Mechi
nyingine itakayochezwa Machi 11 mwaka itakuwa kati ya Polisi Dodoma na Kagera
Sugar. Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Jumatano ya
Machi 14 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Simba watakuwa wageni wa Polisi
Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati Yanga watakuwa wenyeji wa
African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
WAZIRI
KUZINDUA TIGO PESA YA TWIGA STARS
Naibu Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala anatarajia kuwa
mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kuchangia timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars)
kupitia Tigo Pesa.
Uzinduzi huo wa akaunti maalumu ya Twiga
Stars kupitia mtandao wa Tigo utafanyika kesho (Machi 10 mwaka huu) saa 5 kamili
asubuhi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na unafanywa chini ya uratibu wa kampuni
ya Edge Entertainment.
Twiga Stars iko kwenye mashindano ya Kombe
la Afrika kwa Wanawake (AWC) ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini
Addis Ababa.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface
Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF)

No comments :

Post a Comment