Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 16, 2012

WANAWAKE 6 WAFUZU MAFUNZO YA UMEME WA JUA, INDIA

ErastoT.
Ching’oro- Msemaji Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Mapema mwezi septemba, 2011, wanawake sita kutoka Wilaya
ya Mtwara 94) na Lindi (2) walichaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Ufundi wa
Kuunganisha Umeme Juan a Matengenezo katika Chuo cha Barefoot kilichoko nchini
India kwa muda wa miezi sita. Mafunzo hayo yamehitimishwa na wanawake
walioshiriki mafunzo hayo wamerejea siku ya Ijumaa tarehe 16 Machi,
2012.

Wanawake hao sita ni Esha M. Mwangana Fatina M. Mzungu
(Lindi); Amina H. Nachingulu, Arafa M. Halfani, Mariam I. Luwongo, Sofia h.
Mnandi na Amina H. Nachungulu (Mtwara); ambao walipokelewa na Kaimu Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bibi
Judith Kizenga, na Mwakilishi Mkazi wa UN Women nchni Tanzana Bibi Anna Falk-
Collins ambao waliongozana na maafisa wengine.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na UN Women kwa ushirikiano
na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na kupatiwa msaada wa
kiufundi chini ya Mpango aw Kutoa mafunzo wa Serikali ya India nchini Tanzania.
Mpango wa Chuo cha Barefoot India wa kuwajengea uwezo “Wanawake Vijijini
Kuimulika Afrika” ni sehemu ya program ya utekelezaji wa mpango wa Un Women
katika kusaidia maendeleo ya wananawake nchini Tanznaia.

Un Women ni sehemu ya Shirika la Umoja wa Mataifa ambalo
utekeleza shughuli zake chini ya mpango wa kuendeleza mazingira na kukuza uwezo
wa kiuchumi kwa wanawake. Mfunzo haya kwa wanawake mafundi wa umeme jua unalenga
kutoana fursa za elimu kwa wanawake ili kukuza shughuli zao za kiuchumi na
kuongeza vipato kwa maslahi ya maisha yao na familia kwa ujumla.

Mpango huu unaendeleza ujumbe maalum wa Kamati ya Hali
ya Wanawake na Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani wenyekaulimbi inayosema
kuuwa “Wawezeshe wanawake Vijijini; Ondoa Njaa na Umaskini”.

Baada ya mafuzo hayo ya miezi sita wakufunzi wanaofuzu
uhandisi wa umeme jua kutoka Chupo cha Barafoot wanatarajiwa kurejea katika
vijiji vyao na kuanzisha miradi ya kuweka umeme jua katika majumbani, na
watawajibika kufanya matengenezo ya mitambo hiyo kwa kwa kipindi cha miaka
mitano.Wahandisi wa umeme jua wa Chuo cha Barefoot wana nia thabiti ya kudumisha
na kuendeleza teknolojia ya umeme jua vijijini.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa
kushirikiana na Chuo cha Barefoot na serikali ya India ina mpango wa kuanzisha
kituo cha kutoa mafunzo ya umeme jua kwa wanawake wa vijijini katika Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi Mtawanya wilaya ya Mtwara vijijini ili kusambaza taaluma
hii katika familia nyingi zaidi.

No comments :

Post a Comment