MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni
Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania
(TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es
Salaam.Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10
likiratibiwa na TPBO.Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa
mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza
kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa
aliokuwa nao."Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na
hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu,"
alisema Galile.Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua
mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado
ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa."Ninauwezo, nimejipanga na
ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa,"
alisema.Naye kwa upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo
ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa
Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndio
utakuwa kwake akisubiri mpinzani
Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za
Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander
Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj
Jones na wengine wengi
Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya
kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo
Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini,
Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo
watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua
sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka
sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani
Akichanganya na mabondia wa Nchini.
No comments :
Post a Comment