Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, March 15, 2012

TBF NAYO YASIMAMISHA WACHEZAJI, VIONGOZI


KAMATI ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF),
imewafungia baadhi ya
wachezaji, viongozi na waamuzi kwa utovu wa nidhamu na
ukiukwaji wa taratibu za
mashindano.
Katibu Msaidizi wa
TBF, Michael
Maluwe, amesema utovu huo wa nidhamu ulifanywa na wahusika wakati
wa michuano
ya Kombe la Taifa, iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo
Kamati ya
Utendaji iliyoketi hivi karibuni jijini Dar es Salaam ilitoa maamuzi
hayo
baada ya kikao chake cha kupitia ripoti za michuano mbalimbali
.
Alisema
viongozi
watatu wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Rushemeza, Henry Kizinja
William na Tito
Nyalalu wamefungia mwaka mmoja kwa lugha za kebehi, vitisho
na matusi kwa
watendaji wa TBF, pamoja na kulazimisha na kushawishi timu
zigomee michuano
katika vikao halali.
"baada ya mechi
viongozi hao
walivuruga taratibu za kikao wakishinikiza kulipwa fedha,
hivyo
hawataruhusiwa kushiriki au kuongoza timu ndani na nje
ya
nchi"Alisema.
Alisema, kamati hiyo
pia ilijadili hali iliyotokea
katika uwanja wa Leaders ya Kocha Msaidizi wa Mkoa
wa Mwanza, Amri Mohamed,
kutokana na kufanyika vitendo vya utovu wa nidhamu
walipocheza na
Unguja.
Alisema pamoja na
Mwanza kugomea mechi ya kusaka mshindi wa tatu
kwa wanaume, pia ilikaidi adhabu
iliyopewa na TBF baada ya kuvunja kanuni za
michuano hiyo kuhusu usajili wa
wachezaji ambapo waliingiza wachezaji wa timu
yao uwanjani wakati wa mchezo wa
fainali huku timu mbili husika katika mchezo
huo zikijiandaa
kukaguliwa.
"Kitendo hicho
kiliashiria kuleta vurugu na
uharibifu wa amani ya mchezo mbele ya mgeni rasmi,
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara,
hivyo kuitwa polisi wa
ziada kulinda usalama.
Kutokana na vitendo
hivyo, mkoa na viongozi wa
Mwanza wamefungiwa mwaka mmoja kushiriki michuano
yoyote itakayoandaliwa na
TBF, huku katika kipindi hiki
cha adhabu viongozi hao hawataruhusiwa
kushiriki au kuongoza ama kujishulisha
na mpira wa kikapu katika michuano
yoyote, kliniki za mpira wa kikapu, michuano
ya shule kitaifa, kushiriki
mikutano yoyote ya wadau nchini na nje ya
nchi.
Kama hiyo
haitoshi
adhabu hiyo imekwenda pia kwa wachezaji Juma Kisoky, Willison
Masanja,
Shilinde Francis, Amon Sembelya Mohamedi Ally, Amri Mohamedi,
Kizito
Bahati, Ahmed Said, Adam
Jegame, Bundala, Charles, Chacha Tubet,
Shinda Vincent, Enock Charles na Kocha
Robert Mwita.

No comments :

Post a Comment