Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, November 30, 2011

UBWA SALUMU AJIFUA KUMKABILI MUSTAFA DOTO DESEMBA 25


Bondia Ubwa Salum (kushoto) na Omari Bayi wakioneshana umwamba wa kutupa masubwi wakati wa Mazoezi ya Kambi ya Ilala Dar es salaam jana Ubwa anajiandaa na mpambano wake na Mustafa Doto Desemba 25 mwaka huu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

TIGO YAZINDUA SHINDANO LA ZAMU YAKO KUSHINDA


Ofisa Viwango wa Kampuni ya Tigo Pamela Shelukindo Katikati akionesha kipeperushi chenye matangazo ya kuanzishwa kwa promosheni ya zamu yako kushinda Dar es salaam leo wengine kushoto ni Benedict Mponzi na alice Maro

DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko


LONDON,

DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko kujadili uwezekano wa kufanyika pambano kati yao Machi mwakani.

Mpiganaji huyo wa London alitangaza kustaafu ngumi Oktoba mwaka huu lakini amesema kuwa yuko tayari kupigana tena kama atapata nafasi ya kurudiana baada ya kupoteza pambano lake Julai dhidi ya Wladimir Klitschko ambaye ni kaka wa Vitali.

Haye mchezo huo alisema: " Sijaona mkataba lakini kuna mazungumzo yanayoendelea.

"Nilisema kabla kabla ya kustaafu ningependa pambano hilo na kuna tarehe katika Machi ambayo imekuwa ikizungumziwa."

Mabondia hao wazaliwa wa Ukraine wamekuwa wakisema kwua mabalkuanalino yanafanyika ili kuwepo pambano la kuwania ubingwa wa WBC unaoshikiliwa na Vitali, baada ya Haye kupoteza pambano ambalo lilifanya apokwe ubingwa wa IBF/WBO dhidi ya Wladimir mjini Hamburg Julai mwaka huu.

Haye mwenyewe alisema amestaafu ngumi lakini yuko tayari kurejea ulingoni kama atajitokeza mmoja kati ya wanamasumbwi wa familia ya Klitschko.

Kumekuwa na mazungumzo kuwa huenda pambano hilo likafanyike Machi mwakani katika mji wa Dusseldorf Ujerumani.

NMB yazindua Kituo cha Biashara Arusha



Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mercy Sila, akizindua rasmi Kituo cha Biashara kwa wafanya biashara wadogo, wakati na wakubwa wa Benki ya NBC mkoani Arusha jana. Wengine wanaoshuhudia kutoka kushoto ni CEO wa NMB, Mark Wiessing, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Misheck Ngatunga na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema. (Picha na Mpigapicha wetu).

MARIAM RAMADHANI MWANAMITINDO MPYA ALIEPANIA KUWIKA

BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha

BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha


WASHINGTON, Marekani


BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha uzito baada ya pambano lake dhidi ya Lamont Peterson litakalofanyika Washington mwezi ujao kama Timothy Bradley atakataa kupigana naye.


Kwa mujibu wa Dail Mail Khan, ambaye ni bingwa wa dunia uzito wa Light-welter atataka kutwangana na Bradley katika mechi ya kuunganisha mataji.

Bondia mwenye miaka 28, Bradley nsiye anaonekana anaweza kutoa upinzani mkubwa kwa Khan katika uzito wao, lakini amekuwa akionesha kuwa hataki kupigana naye.

Khan mwenye miaka 24, anaamini kuwa kama

Bradley ataendelea kugoma kupigana hatakwua na uamuzi mwingine ataacha na mapambano ya light-welter na mikanda yake na kuhamia katika uzani wa welter ili kupata mechi kubwa.

Kama pambano dhidi ya Bradley litakuwepo kwangu nitabaki katika uzito nilio nao lakini kama halitakuwepo nitahamia katika uzito wa welter,"alisema Khan.

Alisema anataka kupigana na mabondia wapya na na lihi ndilo linamsukuma kwa sasa.

"Tutaona kitu gani kitatokea baada ya mechi hii na kama pambano dhidi ya Bradley litafanyika. kama sivyo nitapandisha uzito."

Khan atapigana Desemba 10 kwenye ukumbi wa Convention Center, Marekani dhidi ya Peterson atakayekuwa nyumbani.

Khan alisema: "Nina mtindo ambao watu wanapenda, kasi na ngumi kali na kweli anamini kuwa ingawa Peterson atakwua nyumbani nitaaungwa mkono zaidi kuliko yeye siku hiyo.

"Hawajapata pambano la kusisimua Washington kwa muda mrefu kwa hiyo itakwua kitu kizuri kwao. Kila wakati nimekuwa nikitamani kupigana katika miji tofauti ili watu kupata nafasi ya kuniona mimi jukwaani.

"Nilitaka kupigana na Bradley na nikaja kupiugana na Marcos Maidana na Zab Judah na kuwapiga wote."

SERENGETI BREWERIES ANZISHENI VIWANDA NJE YA NCHI, PINDA



Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda cha SBL, Mhe. Pinda aisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbali mbali waliokuwepo katika uzinduzi huo.
Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kati) akipiga makofi mar baada ya ufunguzi wa kiwanda hicho, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa EABL, Seni Adetu, na kulia kwake ni Waziri wa Manispaa ya Nairobi, Bw. Njeru Githae ambaye alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu Raila Odinga wa Kenya na wageni wengine waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
---
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameitaka kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd. (SBL)nchini kuanzisha viwanda katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kupanua soko la bia hiyo na kupata faida zaidi.

Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha kisasa cha Serengeti mjini Moshi leo (Jumanne Nov. 29, 2011) Mhe. Pinda alisema Kampuni hiyo lazima ijipanue kama vile wafanyabiashara wengine wa nje wanavyowekeza nchini.

“Kwa vile bidhaa yenu inapendwa hata soko la nje, anzisheni viwanda Burundi au Uganda… wenzetu wa nje wanafanya vivyo hivyo na kuwekeza hapa nchini,” alisema.

Kiwanda cha Serengeti Moshi, ambacho kimejengwa kwa ubia na Kampuni ya Bia ya East African Breweries Ltd. (EABL) ya Kenya ni cha tatu nchini. Vingine viwili vipo Dar es Salaam na Mwanza.

Bia ya Serengeti ilipata tuzo kwa kuwa ya kwanza katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika Ireland hivi karibuni.

Waziri Mkuu pia alisema ataitisha kikao kitakachomjumuisha Waziri wa Kilimo na Chakula na wawakilishi wa Serengeti Breweries ili kuhakikisha namna bora ya kupata kwa uhakika mali ghafi muhimu ya kutengeneza bia, mtama.

Alisema mtama unaweza ukawa biashara nzuri kwa wakulima kwa kuwa Serengeti Breweries wanaununua kwa Sh. 600 kwa kilo moja ikilinganishwa na bei ya mahindi ambayo ni wastani wa Sh. 350 kwa kilo.

“Kuzalisha mtama ni gharama nafuu zaidi kuliko mahindi na kwamba zao hilo linastahamili ukame. Tukutane na Wairi wa Kilimo kuona namna ya kupata zao hili nchini kwa uhakika zaidi,” aliongeza.

Serengeti Breweries inahitaji tani 18,000 za mtama kwa mwaka, lakini upatijanaji wake hauna uhakika, Waziri Mkuu aliambiwa.

Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Manispaa ya Nairobi, Bw. Njeru Githae ambaye alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu Raila Odinga wa Kenya; Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bibi Diane Corner na Mtendaji Mkuu wa EABL, Bw. Seni Adetu.

Mapema, kwenye Ikulu ndogo, mara baada ya kuwasili Moshi, Mhe. Pinda alisomewa taarifa ya mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Leonidas Gama na kusifu jitihada za mkoa za kujietea maendeleo.

JERRY MURO SASA YUPO HURU



Aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro akitoka mahakamani huku akisindikizwa na mkewe Jennifer John (katikati) leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es Salaam kumwachia huru na kuwafutia mashtaka.
Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano mara baada ya Mahakamani kumwachia huru na kuwafutia mashtaka.

Aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa huru na kufutiwa kesi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro akiwa na mkewe Jennifer John huku wakiwa na nyuso za furaha.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es Salaam imemwachia huru na kuwafutia mashtaka aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro pamoja na washtakiwa wenzake wawili ambao ni Edmund Kapama na Deogratius Mgasa waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya tsh.10 milioni.

Aliyekuwa Mtangazaji wa TBC1, Jerry Muro na wenzake 2, wameachiwa huru leo na hakimu Frank Mosha wa mahakama ya kisutu baada ya kuwaona hawana hatia na makosa waliyoshitakiwa nayo. Jerry na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matatu ya Kula njama ya kutenda kosa, kuomba rushwa na kujifanya maafisa wa Takukuru, madai ambayo yametupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi. picha zaidi za tukio zitawajia hivi punde....stay tuned!

Monday, November 28, 2011

Rashid Matumla VS Maneno Osward KUPIMA UKIMWI SIKU KUMI KABLA YA MPAMBANO



Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.

UTasindikizwa na mabondia Venas Mponji atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa

Siku kumi kabla ya mpambano huo mabondia Rashidi Matumla na Maneno Osward wameshauliana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu kama wanatumia sheria za mchezo huo azirusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Rashid Matumla VS Maneno Osward KUPIMA UKIMWI SIKU KUMI KABLA YA MPAMBANO



Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.

UTasindikizwa na mabondia Venas Mponji atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa

Siku kumi kabla ya mpambano huo mabondia Rashidi Matumla na Maneno Osward wameshauliana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu kama wanatumia sheria za mchezo huo azirusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

BAHATI NASIBU MPYA KUANZA DESEMBA MOSI


Mkurugenzi wa Bahati nasibu ya Taifa Talimba Abbasi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu bahati nasibu mpya itakayoanza mwezi ujao kulia na Amani Honestus kutoka kampuni ya kusimamia michezo ya kubahatisha ya WINLOT

MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAENDELEO YA WANAWAKE ZANZIBAR (COWPZ)



Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) Balozi Amina Salum Ally, kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kusimamia Jumuiya hiyo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (wa pili kulia) akikata Keki maalumu iliyoandaliwa ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Wengine ni baadhi ya Viongozi wa Jumuiya hiyo kutoka (kushoto) ni Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo, Vijana Wanawakw na Watoto, Zainab Omary Juma, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Awena Seif na (kulia) ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Balozi Amina Salum Ally. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akijumuika na baadhi ya Kinamama waliohudhuria maadhimisho ya sherehe hizo za miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza na Mkuu wa Kikundi cha Nuru ya Kisauni, Hamisa Maabad Ali, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akipokea maandamano ya Wanawake na Vijana, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

RAIS DK JAKAYA KIKWETE MARA BAADA YA MKUTANO WAKE NA KAMATI YA CHADEMA JANA



Rais Dk. Jakaya Kikwete akiagana na viongozi wa Kamati ya CHADEMA baada ya mkutano wa jana wa na JK na kamati ya Uongozi ya CHADEMA iliyokwenda kumuona kuzungumzia mchakato wa katiba.
Baada ya maongezi marefu yaliyodumu kwa takriban masaa mawili na nusu, mwenyeji aliwakaribisha wageni wake juisi na chai na kahawa kabla ya kuagana nao kwa furaha
na kuwaomba waende tena kesho Ikulu saa nne ili baada ya kujadiliana na timu yake ya Serikali, maongezi yaendelee
Rais Dk Jakaya Kikwete akiagana na mmoja wa wanakamati huku Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akifurahia jambo.

Rais Dk Jakaya Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akisalimiana na viongozi wa Serikali na Mawaziri waliohudhuria katika kikao hicho.

Rais Dk Jakaya Kikwete akifurahia jambo wakati alipokuwa akiongea na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
Rais Dk Jakaya Kikwete akifurahia akizunguma n akamati hiyo jana.
Rais Dk Jakaya Kikwete akimpa glasi ya juisi Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe.

Rais Dk Jakaya KikweteJakaya Kikwete na ujumbe wakiwa katika mkutano na kamati ya CHADEMA jana Ikulu jijini Dar es salaam.

Thursday, November 24, 2011

WATANZANIA WAWILI KUCHEZA LIGI DARAJA LA PILI SWEDEN




Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)

Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/

FAINALI UHAI CUP YASOGEZWA

Release No. 123
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 25, 2011
FAINALI UHAI CUP YASOGEZWA
Mechi ya fainali ya michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Kombe la Uhai (Uhai Cup) kwa klabu za Ligi Kuu sasa itachezwa kesho (Novemba 26 mwaka huu) saa 3.00 asubuhi kwenye Uwanja wa Karume.
Awali fainali hiyo kati ya Simba ambayo iliingia hatua hiyo kwa kuitandika Toto Africans mabao 4-1 na Azam iliyofuzu kwa kuizamisha Serengeti Boys (timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17) mabao 3-0 ilikuwa ichezwe leo (Novemba 25 mwaka huu) saa 9.00 kwenye uwanja huo.
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi za michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza leo (Novemba 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa. Kila siku kwenye michuano ya Chalenji zinachezwa mechi mbili; ya kwanza saa 8.00 mchana na nyingine saa 10.00 jioni.
Michuano ya Kombe la Uhai inadhaminiwa na Kampuni ya S.S. Bakhresa kupitia maji Uhai ambapo bingwa atapata sh. milioni 1.5, mshindi wa pili sh. milioni moja wakati wa tatu atapata sh. 500,000. Mbali ya fedha hizo, bingwa atapata medali za dhahabu, makamu bingwa medali za fedha na mshindi wa tatu medali za shaba.
Mchezaji bora sh. 400,000, mfungaji bora (sh. 300,000), kipa bora (sh. 300,000) na timu yenye nidhamu sh. 300,000.
VIINGILIO MICHUANO YA KOMBE LA CHALENJI
Viingilio kwa mechi za hatua ya makundi kwa michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza leo (Novemba 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam vitakuwa kama ifuatavyo;
Kwa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni zaidi ya 30,000 kiingilio kitakuwa sh. 1,000 wakati viti vya rangi ya chungwa ambavyo ni zaidi ya 10,000 kiingilio kitakuwa sh. 3,000. VIP C na B ambayo jumla ya viti vyake ni 8,000 kiingilio kitakuwa sh. 5,000 wakati VIP A yenye viti 700 kiingilio ni sh. 10,000.
Powered by Sorecson : Creation de site internet
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Awarusha Wakaazi wa DMV

Mwana muziki wa kizazi kimpya ndani ya Washington DC, AJ Ubao wa kwanza (kushoto) pamoja mzee wa kuwachanganya Dmk global Dickson Mkama. wa kwanza( kulia) wakiwanyumba ya jukwa na mwana muzingi aliekuwa anasubiriwa kwa hamu siku ya jana Jumatano Nov23, 2011 katika sherehe za Thanksgiving Muimba Jose Chameleone katikatia, akisubiriwa kwa hamu na wapenzi wake


Nyuma ya jukwa mwana dada Luren akipata flash ya pikee kabla ya unyesho kuanzaa


Muimbaji Ana Lov akipata flash ya pamoja na rafiki yake kwenye onesho hilo la Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone.


Cheif wa swahilivilla Abou Shatry akipata picha ya pamoja na kundi zima la muimbaji kutoka Uganda Jose Chameleone.


Aj Ubao alikuwa ni mumbaji wa pili kuimba katika onyesho hilo waliosherikiana na mwanamuziki wa kutoka Uganda Jose Chameleone, wakiwa nyuma ya jukwa akipata flash ya pamoja na mdhamin wake wapendo


Wapenzi wa tazamaji wakisubiri kwa hamu onyesho hilo kuazarasmi ndani ya ukumbi wa Rendezvous mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.S


Mwana muziki wa kizazi kimpya kwa muziki wa R&B ndani ya Washington DC, AJ Ubao akiwarusha vibaya sana wapenzi wa muziki wa nyumbani wanaoishi hapa DMV Jana jumatano Nov 23, 2011 Nchini Marekani.


Wapenzi wa muziki wakinyumbani wakiwa wanamshangaa Msanii wa hapa Washington DC, AJ Ubao


Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone akifanya vituz vyake ndani ya Rendezvous Hall mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.S


Mamia ya watu jana walifurika kuja kumuangali Msanii kutoka Nchini Uganda kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimba zake, ikiwemo mama roda, Jamalila analia, na nyingi nyenginezo.


Mamia ya warembo waliohudhuria kwenye Show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone

Warembo mikono juu wakiwa wamevudiwa na uwimbaji wa mwanamuziki huyo ndani ya ukumbi uliofurika warembo wa Kiafrica.


Juu na chini full warembo wakipata hisia za muziki wa muimbaji maarefu kutoka nchini Uganda Jose Chameleone.


Sauti ya muimbaji Jose Chameleone inayofurahisha warembo wamuziki wa kinyumbani


Kama kawaida yake akiwa na kundizima ndani ya Washington DC Jana Jumatano Nov 23,2011


Wakati mwengine warembo hupandwa na jazbaba wale wanaposhindwa kujizuwia na kuomba mic ili kuchombeza wimbo uliokuwa unaimbwa hewani wa kipepo


Mambo ya jana hayo cheza ni kucheze ndani ya Rendezvous Hall


Mapozi na wewe: mrembo akipata picha kutoka kwa mpiga picha wetu


Hivyo ndiovyo ilivyoo hakuna fitina


Cheza nikucheze juu na chini warembo wa Kiganda ndani ya Nyumba


Mrembo aleehudhuria ndani ya unyesho hilo kabambe la Muimbaji Kutoka Nchini Uganda Jose Chameleone


Kwakweli ilikuwa sho ya aina yake wapenzi wengi ambao ni Waganda aliofurika na kumuunga mkono jamaa yao


Mwana mitindo wa Uganda jina lake hatujaweza kulipata vyema lakini ni Mwanamitindo wa Uganda!


Cheza ni kuche hiyo huku warembo wakipata flashi ya pamoja kwenye show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Alivyo warusha Wakaazi wa DMV Jana Nov 23, 2011 kwenye siku kuu ya Thanksgiving Nchini Marekani. Picha zote na http://swahilivilla.blogspot.com/