Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, November 11, 2011

RASHIDI MATUMLA NA MANENO OSWARD KUZIPIGA DESEMBA 25



Na Mwandishi Wetu MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa. Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam . Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa habari wa Kampuni Adios Promotion ambao ndio waandaaji wa pambano hilo, Mao Lofombo alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao. Alisema tayari mabondia hao wamekubali kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la marudiano na kwamba wameshaanza maandalizi ambapo kila mmoja amejigamba kumstaafisha mwenzie ngumi. Mao alisema, licha ya pambano hilo linalotarajia kuvuta hisia za mashabiki wa ngumi, pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Rashidi Ally atachapana makonde na Hassan Sweet, Kalulu Bakari na Athuman Kalekwa na Shabani Kazinga na Kashinde Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali. '' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani, DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments :

Post a Comment