Aliyekuwa  Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry  Muro akitoka  mahakamani huku akisindikizwa na mkewe Jennifer John  (katikati) leo  baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es  Salaam  kumwachia huru na kuwafutia mashtaka.
   Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano mara baada ya Mahakamani kumwachia huru na kuwafutia mashtaka. 
   Aliyekuwa  Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro  akifanya  mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa huru na   kufutiwa kesi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es   Salaam.
    Aliyekuwa  Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry  Muro akiwa na  mkewe Jennifer John huku wakiwa na nyuso za furaha.
   Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es Salaam imemwachia  huru na  kuwafutia mashtaka aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji   Tanzania (TBC) Jerry Muro pamoja na washtakiwa wenzake wawili ambao ni   Edmund Kapama na Deogratius Mgasa waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya   kuomba rushwa ya tsh.10 milioni.
  
Aliyekuwa   Mtangazaji wa TBC1, Jerry Muro na wenzake 2, wameachiwa huru leo na   hakimu Frank Mosha wa mahakama ya kisutu baada ya kuwaona hawana hatia   na makosa waliyoshitakiwa nayo. Jerry na wenzake walikuwa wakikabiliwa   na mashitaka matatu ya Kula njama ya kutenda kosa, kuomba rushwa na   kujifanya maafisa wa Takukuru, madai ambayo yametupiliwa mbali kwa   kukosa ushahidi. picha zaidi za tukio zitawajia hivi punde....stay   tuned!
No comments :
Post a Comment