Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Tabora, Henry Mwakasendo (wa pili kulia) akikabidhi funguo ya jengo la bweni la wanafunzi wenye ulemavu la Shule ya Msingi Sikonge, lililojengwa na NBC kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sikonge ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Moshi Chang’a, shuleni hapo Mkoani Tabora leo. Bweni hilo pamoja na ukarabati wa madarasa mawili ya shule hiyo vimeigharimu NBC kiasi cha shs milioni 67. Kulia ni Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja na wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa benki hiyo, Addie Mhina.
Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (wa tatu kushoto) na Ofisa Uhusiano wa benki hiyo, Addie Mhina (kushoto) wakizungumza na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili wa Shule ya Msingi Sikonge katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa jengo la bweni kwa ajili ya wanafunzi hao na madarasa mawili yaliyokarabatiwa vyote vikiwa na thamani ya shs milioni 67 katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Sikonge, Tabora leo.
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Tabora, Henry Mwakasendo (wa pili kulia) akishikana mikono na mtoto mwenye ulemavu, Damiel Gilbert katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa jengo la bweni la wanafunzi wenye ulemavu la Shule ya Msingi Sikonge, shuleni hapo Mkoani Tabora mwishoni leo. Bweni hilo pamoja na ukarabati wa madarasa mawili ya shule hiyo vimeigharimu NBC kiasi cha shs milioni 67. Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano w NBC, Eddie Mhina Mshauri wa Mambo ya Habari Redemptus Masanja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sikonge ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Moshi Chang’a.
No comments :
Post a Comment