MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI BARAZA LA IDD NA SWALA YA ID KITAIFA MSIKITI WA AL FAROUK DAR
 
 
   
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya Baraza la Eid El-Haj, baada ya swala ya Idd iliyofanyikaKitaifa  kwenye Msikiti wa Al farouq Kinondoni jijiji Dar es Salaam leo Novemba 6. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal Wa pili (kulia) Rais Mstaafu wa Comoro,  Mohammad  Abdallah Sambi (kulia) Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Muhidin Mkoyogole na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakijumuika na waumini wa dini ya kiislam katika swala ya Eid El Haj, iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd katika Msikiti wa Al Farouk, uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akimpokea Rais Mstaafu wa Comoro, Mohammad  Abdallah Sambi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba  na Baraza la Idd. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akipokelewa na mmoja wa waumini wa dini ya Kiislam, Asha Baraka, wakati alipowasili alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na  Baraza la Idd. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislam kuomba dua baada ya swala ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa aL Farouk Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa kwanza (kulia) akishiriki Swala ya Idd El Haj, iliyoswaliwa katika Msikiti wa Al Farouk uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6. Mbele ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Muhidin Mkoyogole, akiswalisha swala hiyo iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba Baraza la Idd. Picha na Muhidin Sufiani-OMR  
 
 
 
                        
                    
 
  
 
 
 
No comments :
Post a Comment