KAMPUNI inayoandaa mashindano Miss International Tanzania, Compass Communications imesema kuwa kukosekana kwa vigezo maalum ndiyo sababu kubwa ya kuamua jujitoa katika mashindano hayo ya kimataifa.
Mkurugenzi wa Compass Communication, Maria Sarungi amesema hayo mara baada ya kuwasili kutoka Chengdu, China ambako mrembo Nelly Kamwelu aliiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo.
Maria amesema kuwa ameshangwa na waandaaji wa mashindano hayo kushindwa kuweka wazi vigezo vya kuchagua mshindi kwani tokea Nelly aingie katika mashindano hayo, hayawahi kufanyiwa usaili wa ina yoyote kinyume na utaratibu.
Amesema kuwa mashindano hayo ambayo yamedumu kwa kipindi cha miaka 51 sasa, hakuna hata mrembo wa bara la Afrika aliyewahi kuingia hatua ya 15 bora, jambo ambalo wameona bora kujitoa kwani yanaonekana kuwa yana ‘ubaguzi’ wa rangi.
Amefafanua kuwa mashindano hayo yanaoandaliwa na kampuni ya Kijapani ya International Cultural Association (ICA) yalishirikisha zaidi ya warembo 60 na kati ya hao, Afrika iliwakilishwa na warembo watatu japo katika mtandao walionyesha jumla ya warembo sita kutoka bara la Afrika.
“Sababu kubwa ni maamuzi ya nchi nyingi za kiafrika kujitoa kutokana na matatizo ambayo warembo wao wamekumbana nayo na kukata tamaa, sisi tumevumilia sana, lakini sasa tumefikia kikomo na tunaomba serikali ilisitoe ushirikiano tena na waandaaji hao,” alisema Maria.
Amesema kuwa Tanzania ilipata kibali cha kushiriki katika mashindano hayo tokea mwaka 2005, lakini wameona ni kupoteza muda kutokana na mambo ambayo yanafanyika.
Kuhusu mashindano ya mwaka huu, Nelly amesema kuwa ameshangazwa sana kutokana na kufanya vyema katika maonyesho ya vipaji, lakini alinyimwa ushindi katika hatua ya mwiso na mrembo kutoka China alitangazwa kutwaa taji hilo.
Amesema kuwa yeye alifanya vyema baada ya kucheza Bellydance na kila mara alikuwa anaitwa kuonyesha shoo katika maeneo mbali mbali tofauti na matokeo.
Foto tofauti za Miss International, Nelly Kamwelu na Mkurugenzi wa Mkurugenzi Compass Communications, Maria Sarungi.
No comments :
Post a Comment