
Waziri   wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka wa pili kutoka kulia    akiangalia ramani halisi inayoonyesha maeneo ya wazi wakati alipokagua   maeneo ya wazi  yaliyovamiwa na wananchi maeneo ya Sinza E wilaya ya   Kinondoni, ambapo pia alikuwa akikagua mabango yaliyowekwa kwa ajili ya   kuataarifu wananchi na kuwaelimisha maeneo ambayo ramani inaonyesha  yako   wazi  kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali. 

Diwani   wa Sinza Bw. Renatus Pamba akimuonyesha Waziri wa Ardhi Nyumba na   Makazi Prof. Anna Tibaijuka maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi   katika maeneo ya Sinza E wengine ni waandishi wa habari walioongozana na   Waziri Tibaijuka. 
  
Waziri   wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka  akizungumza na   waandishi wa habari mara baada ya kukagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na   wananchi katika maeneo ya Sinza E leo mchana. 

Waziri   wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mkazi wa   Sinza Ndahani Yohana ambaye amenunua eneo la wazi kwa utapeli kwa   shilingi milioni 500 wiki mbili zilizopita, ambapo ramani halisi   inaonyesha eneo hilo ni la wazi. 
 
 
No comments :
Post a Comment