
Kocha   wa timu ya taifa Taifa Stars Jan Paulsen akizungumza na waandishi wa   habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo, mara baada ya   timu hiyo kuwasili ikitokea N'Djamena nchini Chad, ambako ilicheza na   timu ya taifa ya nchi hiyo na kuifunga magoli 2 kwa 0.   Timu hizo  zitarudiana siku ya jumanne wiki hii kwenye uwanja wa Taifa  jijini Dar  es salaam, Taifa Stars inahitaji ushindi au sare ya aina  yoyote ili  kuingia katika hatua ya makundi kwa ajili ya kinyang'anyiro  cha  kushiriki kombe la dunia  mwaka 2014 nchini nchini Brazil. 

Kulia   ni Mchezaji wa Taifa Stars Nizar Khalfan na kushoto ni Henry Joseph   wakiongoza wenzao wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu   J.K.Nyerere leo jijini Dar es laam wakitokea nchini Chad. 

Kocha   wa timu ya taifa Taifa Stars Jan Paulsen akiingia kwenye basi la timu   hiyo, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere DIA   jijini Dar es salaam. 

Golikipa watimu ya taifa Juma K. Juma akiwa katika pozi katika basi la Taifa Stars leo. 

Mkurugenzi   wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) Teddy   Mapunda na Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo kushoto,   wakiwapongeza wachezaji wa Taifa Stars, mara baada ya kuwasili kwenye   uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo alasiri. 

Mwandishi   wa habari wa BBC nchini David Eric Nampesya akimhoji katibu mkuu wa   Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Angetile Osiah wakati wa   mapokezi ya Taifa Stars iliyowasili nchini leo ikitokea nchini Chad. 

Mwandishi   wa habari wa BBC nchini David Eric Nampesya akipozi kwa picha na   Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers   (SBL) Teddy Mapunda. 

Mzungu   huyu ambaye hakufahamika jina lake mara moja, akipata taswira baada ya   kuvutiwa na vijana hawa wanaofanya kazi ya promosheni ya bia ya   Serengeti Lager. 
Wachezaji   hawa wa kesho nao wameshiriki kuwapokea kaka zao Taifa Stars  wakati   walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo. 
Mashabiki mbalimbali wamejitokeza kuja kuwapokea wachezaji wa timu yao Taifa Stars ilipowasili leo ikitokea nchini Chad.     
No comments :
Post a Comment