Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama Cha Kikomunisti cha China Liu Yunshan baada ya mazungunzo yao Ikulu mjini Dar es Salaam, jana. Walioko nyuma, kutoka kiushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa (wapili kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama (kulia) na wengine ni Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Martine shigella, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, Katibu wa NEC, Mambo ya Nje Januari Makamba na Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma.
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi Chama Cha Kikomunisti cha China, Liu Yunshan (wapili kulia) akipatiwa maelezo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kichina ya StarTimes William Lan alipotembelea kampuni hiyo, Mwenge, Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Watatu kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye ambao walifuatana na kiongozi huyo.
Nape akiungana na wasanii wa kundi la Tanzania House Of Talent (THT) kucheza ngoma, kundi hilo lilipokuwa likiyumbuiza katika ziara ya Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi Chama Cha Kikomunisti cha China Liu Yunshan (hayupo pichani) kwenye ofisi za kampuni ya StarTimes, Mwenge Dar es Salaam, jana
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimtuza fedha msanii Hassan Kasim wa kikundi cha Tanzania House Of Talent baada ya kuvutiwa na uhodari wa kucheza sarakasi wa msanii huyo, kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika ziara ya Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi Chama Cha Kikomunisti cha China Liu Yunshan (hayupo pichani) kwenye ofisi za kampuni ya StarTimes, Mwenge Dar es Salaam, jana.
No comments :
Post a Comment