Mkurugenzi   wa Mashindano katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw.  Saad  Kawemba akizungumza wakati wa kliniki ya mashindano ya Shirikisho  la  Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA yanayojulikana kama  (TUSKER  CACAFA CHALLENGE CUP 2011) inayofanyika kuanzia asubuhi hii  kwenye  ukumbi wa mikutano wa DICC PPF Tower jijini Dar es salaam,  ambapo  waandishi wa habari  watakaoandika habari za mashindano hayo  kutoka nchi  mbalimbali ukanda wa Afrika Mashariki wanahudhuria na  kupata maelezo  mbalimbali . 
Katibu   Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Bw.   Nicholas Musonye akitoa mada katika Kliniki hiyo, mbele ya waandishi wa   habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka ukanda wa Afrika   Mashariki. 
Kulia   ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki   CECAFA Bw. Nicholas Musonye na Meneja wa bia ya Tusker inayozalishwa na   kampuni ya Serengeti Breweriers Ritah Mchaki wakifuatilia jambo, wakati   Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF Saad Kawemba alipokuwa akitoa mada  yake  na kukaribisha waandishi  mbalimbali waliokuja nchini kwa ajili ya   kuandika habari za mashindano ya TUSKER CACAFA CHALLENGE CUP 2011. 
Washiriki wa Kliniki hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyokuwa yakitolewa na watoa mada katika kliniki hiyo.  zaidi tembelea http://fullshangwe.blogspot.com/ 


No comments :
Post a Comment