Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, May 28, 2010

TIMU ZA TAIFA ZA AFRIKA KATIKA KOMBE LA DUNIA

Kocha wa timu ya taifa ya Misri Hassan Shehata bila shaka amejipatia umaarufu mkubwa kabla na hata wakati huu tukielekea katika kombe la dunia. Hakika sio tu kwa sababu hivi sasa anaogelea katika dimbwi la pongezi nyingi, bali ni kwa sababu makocha maarufu duniani wangependa sana kuchota sehemu ya maarifa na umahiri wake.
Shehata

Hassan Shehata akipongezwa

Shehata mwenye umri wa miaka 60, alifanikiwa ‘kuzitandika’ si chini ya timu nne zinazotarajiwa kuiwakilisha Afrika katika kombe la dunia wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika iliyofanyika mwezi wa kwanza nchini Angola na kutwaa ubingwa. Timu hizo ni Nigeria, Cameroon, Algeria na Ghana. Nigeria wao baada ya kumtimua kocha Shaibu Amodu, wakaamua kufuata hekima ya kutafuta maarifa toka kwa wapinzani wao ( if you can’t beat them, join them”) na kuonesha nia ya kumpa Shehata kazi hiyo yenye changamoto nzito. Hata hivyo inaonekana kuwa jitihada hizo zimekutana na ukuta mgumu wa Chama cha soka cha Misri.

Hakika si mengi tunayoweza kujifunza katika soka dhaifu la Nigeria wakati wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika na hatimaye kufukuzwa kwa Amoadu ukilinganisha na timu zingine zitakazoiwakilisha Afrika katika Kombe a Dunia. Ilichapwa na Misri, ikabahatika kwa Benin, ikapata ahueni kwa Msumbiji lakini ikawa dhaifu mbele ya Zambia na kulewa mbele ya Ghana. Hakika hatuwezi sema kuwa Soka la Nigeria wakati wa fainali hizo lilikuwa lenye uwezo wowote wa maana.

Nigeria

Kikosi cha Nigeria kilichoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2010

Picha-caption-Nigeria ilishika nafasi ya tatu lakini ikaamua kumtimua kocha

Nigeria wanaonekana kawaida kuanza vyema lakini hakika wanahitaji sana kuongeza msuli ili mambo yao yaweze kufanikiwa.

Kushindwa kufunga magoli lilikuwa tatizo wakati mwingine. Yakubu na Obafemi Martins walikosa magoli mengi. Lakini tatizo hasa ni kukosekana kwa kwa kiungo mchezeshaji Viungo wengi walioichezea Nigeria katika fainali hizo ni viungo wakabaji; John Obi Mikel, Dickson Etuhu, Sani Kaita na Yussuf Ayila, hali iliyosababisha mshambuliaji Osaze Odemwingie awe na kazi kubwa.

Nigeria wana tatizo jingine la kutocheza kama timu moja iliyoshikamana. Ni kikosi kilichojaa ubinafsi wa mchezaji mmoja mmoja. Hii itakuwa ni changamoto kubwa kwa kocha mpya hasa ukitilia maanani muda mfupi uliobaki kabla ya Fainali za Kombe la Dunia na timu pinzani katika kundi B ambazo ni Argentina, Korea ya Kusini na Ugiriki.

Wachambuzi wa soka kwa muda mrefu wamekuwa wakilisema jambo hilo kuhusu Nigeria lakini si kwa Ivory Coast.

Kama ilivyo kwa ndugu zao hao wa Afrika Magharibi, kikosi cha Ivory Coast nacho kilikosa kiungo mchezeshaji. Japo Yahya Toure na Didier Zokora ni viungo hodari lakini hawakuonesha kuelewana ipasavyo au uwezo wa kubadilisha mchezo. Jukumu hili linaonekana kuwaaangukia Abdulkader Keita na Bakary Kone, lakini kule Angola hawakuonesha la maana sana. Ukimtaja Gervinho, bado hakuweza kuonesha makeke licha ya matarajio makubwa aliyotwishwa.

Drogba

Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba

Hiyo ni kwa upande wa ubunifu katika kiungo.Lakini udhaifu wake hatuwezi kuulinganisha na udhaifu mkubwa uliojionesha katika nafasi ya ulinzi hasa wakati wa kipigo cha nusu fainali toka kwa Algeria. Mabeki na viungo walipoteza kabisa maelewano, hali iliyojionesha wazi pale beki wa Algeria Madjid Boughera alipotumia vyema udhaifu huo kufunga goli la muhimu la kusawazisha katika dakika ya 92.

“Timu kubwa haziachii ushindi wa 2-1 upotee kirahisi kunapokuwa kumebaki dakika chache mechi kumalizika”, akasema kocha wa Ivory Coast kutoka Bosnia Vahid Halilhodzic. “Tulikuja na matumaini makubwa, lakini kwa mara nyingine Ivory oast imeshindwa kutoa matokeo mazuri. Si tatizo la kimwili ila ni la kisaikolojia”

Lilikuwa ni tatizo la kisaikolojia au ni matokeo ya pumziko refu la siku tisa lililosababishwa na kujiondoa kwa Togo? Wachambuzi wanaweza kusema ni tatizo la kisaikolojia, wakizingatia matokeo mabaya ya miaka ya nyuma. Mwaka 2006 Ivory Coast ilifungwa na Misri katika fainali, ikapoteza nusu fainali mwaka 2008 mbele ya hao hao Misri na mwaka huu ikabanwa mbavu na Algeria.

Inavyoonekana ni kuwa Ivory Coast hupata wakati mgumu ikikumbana timu zilizojipanga vyema. Sifa ambayo timu za Afrika Kaskazini wanayo. Lakini bora wajue kuwa wapinzani wao ndani ya kundi G, Korea ya Kaskazini, Ureno na Brazil, zote zina sifa hiyo hiyo ya kujiandaa na kujipanga vyema. La kutia hofu zaidi ni kwamba mashabiki wa Ivory Coast wanaonekana kupoteza imani yao kwa mshambuliaji Didier Drogba ambaye kiwango chake kule Angola kiliwakasirisha wengi.

Sina hakika kama watu wa Cameroun wana hisia na mawazo hayo hayo juu ya Samuel Eto’o. Lakini naye hakuwa katika kiwango chake kule Angola. Kocha Paul Le Guen alimchezesha nyuma ya washambuliaji wawili mbele katika kipigo cha robo fainali kutoka kwa Misri. Lakini kwa silika ya kiwindaji aliyo nayo Eto’o, inakuwaje achezeshwe katika nafasi hiyo?.

Eto'o

Samuel Eto'o wa Cameroon

Kulikuwa na mengi ya kushangaza hasa ukitilia maanani matarajio mengi yaliyowekwa kwa viungo Stephane Mbia na Jean Makoun.

Lakini Mbia alipewa dakika 45 tu na Makoun akaachwa katika mechi dhidi ya Misri. Nafasi hizo wakachukua Enoh Eyong na George Mandjeck mwenye umri wa miaka 21, ambaye aling’ara katika pambano dhidi ya Misri.

“Niliamua kutia damu changa ili kuleta nguvu mpya” akasema kocha Le Guen. “Mechi yetu na Misri ilionesha nilikuwa sahihi”.

Hatimaye kulifanyika mabadiliko katika ulinzi. Rigobert Song hakuanzishwa na vijana wapya Nicolas N’Koulou na Aurelian Chedjou wakakamata nafasi.

Lakini Cameroun wana tatizo la kufungwa mapema. Misri wakaonesha udhaifu wa golikipa Carlos Kameni, licha ya kwamba kwa kawaida huwa huwa ni kizuizi imara golini lakini si kwa Ahmed Hassan.

Rahim Ayew na Hans Sarpei walicheza vyema Angola licha ya vikwazo kadhaa.

Cha kutia moyo ni kuwa wachezaji wote 19 (outfield players) walionja ladha ya kucheza soka Angola ambako mwinuko kutoka usawa wa bahari katika mji wa Lubango ni mita 1750. Hali hiyo itawaweka katika hali ya kukabili mechi za kundi E. Katika mwinuko wa jiji la Bloemfotein dhidi ya Japan ambao ni mita 1400 na dhidi ya Denmark jijini Petoria mita 1275. Mechi ya mwisho dhidi ya Uholanzi itakuwa ni katika usawa wa bahari.

Lakini kama kuna timu iliyofaidika na michuano ya Angola ni Ghana.Wachezaji wake sita wa kikosi cha kwanza walikosekana, wakiwemo wote wa nafasi ya kiungo na walinzi mahiri wawili. Vijana wachanga wa Ghana waliopata nafasi ya kucheza waliikabili michuano kwa ujasiri kiasi kwamba uzoefu huo unaweza kuwasaidia wakati wa kombe la dunia watakapokuwa wakikabiliana na wapinzani wao wa kundi D, Ujerumani , Australia na Serbia.

Hali ya kisaikolojia ya Ghana ilitiliwa mashaka hapo awali lakini vijana kama Kojo Asamoah, Samuel Inkoom, Agyemang Badu na Opoku Agyemang walionesha ujasiri mkubwa wa kuzikabili mechi ngumu na inaashiria hali nzuri ya siku za baadae kwa soka ya Ghana.

Essien

Nahodha wa Ghana, Michael Essien

Timu ya Ghana imejengwa kutokana na kikosi cha vijana wa chini ya miaka 20 walionyakua kombe la dunia. Vijana sita kati ya walionza katika fainali dhidi ya Misri walikuwa na miaka 22 au chini. Lakini kwa kombe la Dunia inaweza isiwe rahisi kukamata nafasi ya kucheza. Hiyo ni kwa kuwa pia zile tofauti kati ya kocha Milovan Rajevac na Sulley Muntari zimemalizwa.

“Wanahitajika wachezaji wenye uzoefu kwa ajili ya kombe la Dunia.Tunao kama John Mensah, John Pantsil, Laryea Kingston, Michael Essien na Sulley Muntari. Wapo wengine pia” anasema kocha Milovan.

Baada ya michuano ya Angola, Milovan alilaumu ukosefu wa uzoefu kwa wachezaji wake lakini akasema kuwa anafurahia uzoefu waliopata vijana wale na kuamini kuwa utasaidia wakati wa kombe la dunia. Bila kuogopa kufanya maamuzi makubwa, kocha Milovan alionesha ubora wake pale timu ilipoweza kuingia fainali licha ya kuwa na majeruhi na changamoto nyingi.

Mafanikio yake makubwa ni kuweza kuwajenga wachezaji kucheza ki timu zaidi kuliko ilivyokuwa kwa timu zingine zitakazoiwakilisha Afrika katika Kombe a Dunia. Nani anajua mchango ambao ungetolewa na vijana wazoefu kama akina Essien, Muntari, Pantsil na wengine kama wangekuwa katika hali nzuri ya kuweza kucheza?

Kwa wengine wenye majina makubwa kama vile Drogba, Eto’o na Mikel ilikuwa ni hali ya kusikitisha. Je ni kwa sababu shauku ya kucheza katika kombe la mataifa ya Afrika kumezwa na aina ya maisha wanayoishi huko Ulaya? Au majina yao makubwa na hali ya soka Ulaya inaweza kuwa ndiyo sababu?

Kama siyo, je sababu ni nini? Lolote jibu liwalo naamini soka la Afrika katika fainali hizi za kombe la dunia litakuwa tofauti sana.

Tuesday, May 25, 2010

KOMBE LA DUNIA: IWEJE CONGO HAWAPO

Wakati bara la Afrika likiandaa michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza, kuna jambo moja ambalo halijabadilika: wapenzi wa soka katika nchi za mashariki mwa Afrika na eneo la maziwa makuu wataendelea kuwaza na kuwazua waiunge mkono timu ipi, kwani hakuna nchi iliyofuzu kutoka eneo hilo.

Mara ya mwisho eneo hilo lilipowakilishwa katika kombe la dunia ilikuwa ni mwaka 1974 na nchi ya Zaire, ambayo leo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Zaire ilikuwa nchi ya pili kutoka bara la Afrika kushiriki michuano ya kombe la dunia baada ya Morocco, iliyoshiriki mwaka 1970, lakini Leopards, kama ilivyojulikana timu hiyo ya Zaire, ilikuwa timu ya kwanza kutoka kusini mwa jangwa la Sahara kufuzu kwa kombe la dunia.

Ingawa haijawezekana tena kwa nchi hiyo kufuzu kushiriki kombe la dunia, wachezaji waliokuwa katika timu hiyo ya mwaka wa 74 bado hujivunia hilo mpaka leo.

‘’Kombe la dunia ni kilele cha soka, ndicho kitu ninachojivunia maishani mwangu kwa kushiriki mwaka 74, tulikuwa nchi ya kwanza ya watu weusi kushiriki kombe la dunia, na ni fahari ya kukumbuka siku zote.’’ Mohamed Kalambay, aliyekuwa kipa wa akiba wa Leopards aliambia BBC.

Mohammed Kalambayi

Mohammed Kalambayi anajivunia kuwa mmoja wa wachezaji walioiwakilisha Zaire katika Kombe la Dunia 1974.

Leopards walifungwa mabao 14 katika mechi tatu bila wao kufunga hata moja. Katika mechi yao ya kwanza walifungwa 2-0 na Scotland, kisha wakabugizwa 9-0 na Yugoslavia, na katika mechi yao ya mwisho wakafungwa 3-0 na Brazil.

Mwepu Ilunga alikuwa mlinzi katika timu hiyo, na ijapokuwa anaona fahari kwamba walifuzu kwenda kushiriki kombe la dunia, angali na machungu kuhusu waliokuwa maafisa wa shirikisho la soka Zaire, ambao anawalaumu kwa kuchukua pesa zilizotolewa na shirikisho la FIFA kwa wachezaji, kama mafao ya kushiriki.

‘’ Tulirejea nyumbani bila senti hata moja kama wachezaji. Kabla ya mchuano wetu dhidi ya Yugoslavia tulifahamu kwamba hatutalipwa, licha ya kufahamu kwamba FIFA walikuwa wameshawakabidhi fedha maafisa wetu. Kwanza tulikataa kucheza, na ilipolazimika kucheza, tulitembea tu uwanjani, na ndio sababu tukafungwa mabao 9.’’

Mwepu Ilunga

Mwepu Ilunga anakumbukwa kutoka na kituko cha kuondosha mpira kuepusha free-kick.

Mwepu aanakumbukwa kote duniani kwa kituko alichofanya katika mechi yao iliyofuatia, dhidi ya Brazil. Brazil ilipata free kick hatua chache kutoka lango la Zaire, wachezaji wa Zaire wakaweka ukuta wa ulinzi. Lakini refarii alipopiga kipenga ili Brazil kupiga free kick hiyo, Mwepu aliondoka kutoka ule ukuta wa ulinzi, akaupiga ule mpira na kuuondosha nje.

‘’ Sijuti hata kidogo, nilifanya kwa kusudi. Nilitaka nipewe kadi nyekundu ili niondoke uwanjani. Kwa nini nicheze kwa faida ya maafisa wa chama cha soka cha nchi yetu waliochukua fedha za wachezaji zilizotolewa na FIFA?. Ila sikufaulu , refa hakunipa kadi nyekundu.’’

Bila kufahamika yaliyotokea, lawama nyingi zilielekezwa kwa kocha wa Leopards Blagoj Vidinic kutoka Yugoslavia. Lakini aliyekuwa naibu kocha msaidizi wa timu ya Leopards Kabamba Nicodem aliambia BBC kitendo cha maafisa wa chama cha soka kuwalaghai wachezaji ndicho kilisababisha matokeo mabaya.

Peter Musembi (kushoto) akiwa na Nicodemu Kabamba

Ujuzi na busara za watu kama Kabamba Nicodemu (shati jekundu) unaweza kusaidia kuirejesha Kongo katika mafanikio ya miaka ya 1970.

Kabamba anasema kwa sasa nchi hiyo ina wachezaji wazuri lakini kinachowafanya kushindwa kwenda kushiriki kombe la dunia ni ukosefu wa maandalizi bora.

‘’Ukosefu wa mipango mahsusi ndio umesababisha nchi ya Congo kushindwa kushiriki katika mashindano makubwa kama vile kombe la mataifa ya Afrika na kombe la dunia; bila maandalizi bora huwezi kufanikiwa katika jambo lolote’’. Anasema Kabamba.

Kuna hamasa kubwa ya mpira wa vilabu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo miongoni mwa mashabiki, klabu ya TP Mazembe kutoka mji wa Lubumbashi kusini mwa nchi ndio mabingwa wa sasa wa Afrika, na vilabu vingine kama AS Vita Club na DC Motema Pembe vinavutia wachezaji kutoka nchi zingine.

Timu ya taifa ya nchi hiyo ndiyo mabingwa wa taji la Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani.

Haya yote yanaashiria uzito unaopewa soka katika Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo, lakini swali linasalia kwa nini hawajaweza kurudi tena katika kombe la dunia tangu mwaka wa 1974?

Rais wa shirikisho la soka nchini Congo Constant Omar Selemani anasema ukosefu wa amani katika nchi, hali mbaya ya kiuchumi na kupuuzwa kwa soka ya vijana kwa kipindi kirefu kulikwamisha maendeleo ya soka katika nchi hiyo.

Constantine Omar Selemani

Constantine Omar Selemani rais wa shirikisho la soka la Congo ana jukumu kubwa la kuirejesha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia.

‘’Maendeleo ya soka yanakwenda kulingana na hali ya nchi, kijamii na kiuchumi. Wakati Zaire ilipofuzu kwa kombe la dunia mwaka wa 74 uchumi wa nchi ulikuwa mzuri, lakini tangu wakati huo kumekuwa na matatizo mengi katika nchi.’’

‘’Pia viongozi wa wakati ule walikosa maono ya kukuza wachezaji wapya. Wale wachezaji walioshiriki kombe la dunia walitaka kwenda kucheza soka ya kulipwa katika nchi za nje, lakini Rais Mobutu akawakataza, akawalazimisha kukaa nyumbani. Wengine waliacha kucheza, na kukawa hakuna mpango wa kukuza vijana wengine’’. Anaelezea Bw Selemani.

Rais huyo wa shirikisho la soka nchini Congo, ameahidi kwamba nchi yao itakuwepo kwenye mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Saturday, May 15, 2010

YANGA YAPOKEA OFA YA NGASA


Yanga SC imeonesha kukomaa baada ya kuipokea ofa ya Azam FC na kwa mujibu wa mwenyekiti wake Imani Madega, “wao kama Yanga hawana mpango wa kumzuia Ngasa na mchezaji yoyote atakayependa kuhama kwani kuhama kwao kutatoa nafasi kwa Yanga kusajiri wachezaji wengine nyota.
Suala la Ngasa kusajiliwa Azam FC limezuka kama filamu, na sasa limekuwa likifuatiliwa na wapenzi wengi wa Mchezo wa mpira wa miguu, awali leo mchana, Azam FC imepeleka barua ya kuomba kumsajili Ngasa ikiwa na ofa ya 25 Milioni. Kiasi hiki ni kikubwa sana kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya usajiri wa wachezaji kwani Ngasa amebakisha mwaka mmoja tuu na sheria za FIFA zinamruhusu mchezaji aliyebakisha mwaka mmoja kuunnua mkataba wake kwa kuilipa klabu aliyokuwa akiichezea mshahara wote uliobaki. Lakini Azam FC licha ya kufahamu sheria hiyo bado imeonesha uungwana na nia njema kwa kuamua kutoa ofa nzuri ambayo ni rekodi nchini.
Juma kaseja ndiye anayeshikiria rekidi ya uhamisho ambapo Uhamishowake kwenda Yanga uliigharimu timu hiyo ya Jangwani Milioni 24 na kama deal hili la Ngasa litafanikiwa basi Yanga na Ngasa watakuwa wakishikilia rekodi ya usajiri wa fedha nyingi kwa wachezaji wa ndani.
Gazeti la Mwanaspoti nalo lina habari kuwa, nanukuu “MAMILIONI ya fedha aliyoahidiwa na klabu ya Azam yamemrudisha nyumbani Mrisho Ngassa na jana alitarajiwa kukutana na uongozi wa Yanga na kuwaelezea nia yake ya kutaka kutosajiliwa tena na klabu hiyo msimu ujao.Ngassa alisema jana kuwa ameamua kurejea nyumbani baada ya kuona kuwa fedha alizopewa na APR ya Rwanda ni ndogo zikilinganishwa na zile alizoahidiwa na Azam.'' Kweli tulifanya mazungumzo na APR wiki hii, lakini walikuwa wanasuasua kunipa fedha ambayo niliitaka mimi na nilipofuatwa na Azam wakanieleza dau kubwa zaidi, ndipo nikaona nisipoteze muda bora nije kuzungumza nao, '' alisema Ngassa ambaye amekuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita.Alisema kuwa alitarajia kukutana na uongozi wa Yanga ili kuwaeleza nia yake ya kutua Azam na kuwaweka wazi fedha anazopata na kuwaomba wamruhusu kwani mpira ni ajira kwa sasa.


'
' Kwa sasa mimi ndio najitengenezea maisha yangu mpira ukiisha hapa sijafanya kitu chochote kesho na kesho kutwa nitavyokuwa naomba omba watu wananisema sana, hivyo naomba viongozi wa Yanga wanielewe na kuniruhusu kuichezea Azam msimu ujao,'' alisema.Pia, aliongeza kuwa uamuzi wake anaamini kuwa ni sahihi kutokana na fedha alizoahidiwa kuwa ni nyingi na anaamini kuwa Yanga hawawezi kumsajili kwa fedha hizo hata iweje.

"Ni zaidi ya fedha ambazo walitaka kunipa APR ambao katika maongezi ya mwanzo walikubaliana nami Shilingi 20 na Azam wananipa zaidi ya hapo."Ninawaomba mashabiki wa Yanga wakubaliane na uamuzi wangu huo kwa ajili ya maisha yangu na ukizingatia nimeitumikia kwa miaka mingi timu hiyo tena kwa moyo mmoja hivyo wasiupokee vibaya uamuzi wangu huo," alisema.Alisema hana shida na viongozi wake anaamini pindi watakapokutana na wenzao wa Azam watafika muafaka na kumruhusu kwa moyo mmoja kuichezea timu hiyo ambayo imekuwa na upinzani kwenye ligi msimu uliopita.Hata hivyo, mchezaji huyo alitangaza dau lake kupitia gazeti la Mwanaspoti kuwa yupo tayari kuondoka Yanga endapo klabu inayomtaka iko tayari kutoa Shilingi 40 milioni.

SENYONJO ATUA AZAM FC


AZAM FC ya Dar es Salaam imefanikiwa kumsajiri nyota wa kimataifa wa Uganda ambaye ni mshambuliaji hatari wa timu ya ya Polisi ya Uganda, Peter Senyonjo ambaye alikuwa akihusishwa na Yanga kwa misimu miwili mfululizo iliyopita.
Senyonjo ambaye anatisha kwa kuzifumania nyavu za timu pinzani anatarajiwa kutengeneza partnership ya hatari na John Raphael Boko Adebagoals amabye kama siyo kukosa baadhi ya mechi kutokana na kuwa Israel kwa majaribio basi angekuwa mfungaji bora msimu huu.

kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti, Yanga walikuwa wamepania kumsajili mchezaji huyo msimu wa 2007 na 2008 lakini wakashindwa kutokana na kutokuwa makini kwenye ufuatiliaji lakini wikiendi iliyopita timu ya Azam imemshusha Dar es Salaam na kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja.

Mchezaji huyo mzoefu na tegemeo kwenye timu ya Taifa ya Uganda, alikuwa jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita kukamilisha uhamisho wake na ameshakwea pipa kurejea Kampala.

Meneja wa Azam, Ibrahim Jeshi amesema kuwa kila kitu kimekwenda vizuri na mchezaji huyo amerejea kwao kukamilisha mambo mengine.

Senyonjo amejijengea umahiri mkubwa akiwa na timu hiyo ya Police kwenye michuano ya kombe la kagame na timu ya Taifa katika chalenji.
Wakati huo huo, beki mahiri wa timu ya Taifa Stars Nadir Haroub Canavaro yupo katika hatua za mwisho za kujiunga za Azam FC, Canavaro mwenyewe ameshatamka wazi kuwa dhamira yake ni kuichezea Azam FC msimu ujao

CHELSEA MABINGWA KOMBE LA FA


Carlo Ancelotti ameweka rekodi wakati Didier Drogba alipopachika bao kipindi cha pili na kuizamisha Portsmouth hali iliyoifanya Chelsea kuweka kibindoni makombe mawili, ubingwa wa Ligi ya England na Kombe la FA.

Shuti la Drogba la adhabu ya moja kwa moja alilopiga kiufundi ndio liliamua ushindi kwa Chelsea katika mchezo ambao Chelsea walikosa mabao mengi kipindi cha kwanza ambapo mpira ulikuwa ukigonga nguzo ya goli mara kwa mara ambapo pia timu zote zikikosa kufunga mikwaju ya penalti.

Chelsea ambayo inakuwa klabu ya saba kushinda makombe mawili katika msimu mmoja, kwa mara nyingine ilikuwa na kila jambo la kumshukuru mshambuliaji wao hatari Drogba, ambaye amezidi kuweka rekodi ya kufunga katika michezo sita iliyopia kwenye uwanja wa Wembely huku msimu huu akiwa amefunga mabao 37.

Alifunga dakika chache tu baada ya Portsmouth kukosa mkwaju wa penalti ambapo Kevin-Prince Boateng alipiga mkwaju usio wa kiufundi na kuokolewa na mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech na ule wakati ambapo Pompey ilionekana kurejea kile ilichofanya miaka miwili iliyopita ukipotea.

Chelsea nayo ilikosa kufunga bao la pili kwa kwaju wa penalti baada ya Frank Lampard kuangushwa na Michael Brown na mkwaju wake kwenda nje.

SERENGETI BREWERIERS YAZINDUA BIA MPYA (UHURU PEAK LAGER)
Mwenyekiti wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Jaji Mark Bomani kulia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Shantanu Chitgopkar wakionyesha mfano wa bia ya Uhuru Peak Lager jana mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar es salaam kwenye Hoteli ya Movenpick, bia hiyo kwa sasa inapatikana kwenye baa mbalimbali na ina kilevi asilimia 5.8 haya kazi kwenu watumiaji wa kilaji endeleeni kujimwaga na Uhuru Peak Lager
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Marcio Maximo akiwa na maiwaifu wake.


WADAU KAMA TULIKUWA CHIMBO HIVI!!!

WADAU WA VIWANJANI KAMA TULIKUWA CHIMBO HIVI KWA MAJUMA KADHAA SASA TUNAREJEA TENA

TUMEREJE TENA

NI MAHABARI YA MICHEZO ZAIDI

KARIBU