Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, September 6, 2010

Ghana, Nigeria zashinda Afrika

Lobamba, GhanaTIMU za taifa za Ghana na Nigeria, zimeibuka na ushindi katika mechi za kusaka tiketi ya kucheza fainali za Matiafa ya Afrika zitakazofanyika 2012.Mjini Lobamba, Ghana 'Black Stars', timu inayoongoza katika viwango vya ubira wa soka barani Afrika na iliyocheza fainali za Dunia nchini Afrika Kusini na kutinga hatua ya robo fainali, iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Swaziland.Andre Ayew aliifungia bao la kwanza dakika ya 13, kabla ya Prince Tagoe kuiongezea Ghana bao la pili dakika ya 70 na Hans Sarpei alimaliza bao la tatu dakika ya 81 na kupanda juu ya Sudan katika Kundi I.Nigeria, ambayo ilitwaa pointi moja katika fainali za Kombe la Dunia, iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Madagascar mjini Calabar, mabao yaliyofungwa na Obafemi Martins dakika ya 19 na Michael Eneramo dakika ya 45.Lakini, ushindi huo uliisaidia timu hiyo kushika nafasi ya pili katika Kundi B, nyuma ya Guinea iliyoichapa Ethiopia mabao 4-1 mjini Addis Ababa.Ethiopia walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Umed Ukuri dakika ya 30. Lakini, Ibrahima Yattara aliisawazishia timu yake bao dakika ya 37.Bao la pili la washindi lilifungwa na Karamoko Cisse dakika ya 60 na Kamil Zayatte alimalizia kufunga bao la nne dakika ya 75 na kuifanya Guinea itoke uwanjani na pointi tatu.Katika Kundi A, Liberia na Zimbabwe zilitoka sare ya bao 1-1 na kuiacha Cape Verde Islands kuongoza kundi hilo baada ya kuichapa Mali 1-0 bao 1-0, Jumamosi.Zambia ilikaa juu katika Kundi baada ya kuifunga Comoro mabao 4-0 mjini Lusaka, mechi ambayo ilichezwa baada ya masaa 24 kutokana na kcuhewa kwa waamuzi wa mchezo huo.Rainford Kalaba aliifungia Zambia bao la kwanza dakika ya tano na Fwayo Tembo aliiongezea bao la pili dakika ya 30 na James Chamanga alifunga bao la tatu dakika ya 40.Zambia waliingia kipindi cha pili kwa kulisakama lango la wapinzani wao ambapo dakika ya 83, Emmanuel Mayuka aliifungia bao la nne na kuwafanya Chipolopolo watoke uwanjani wakiwa na furaha.Mechi nyingine katika kundi hilo, Msumbiji na Libya, zilitoka suluhu, mjini Maputo.Mamadou Niang alifunga mabao matatu mjini Lubumbashi na kuiwezesha Senegal kutoka uwanjani kifua mbele wakiwa na mabao 4-2 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).Moussa Sow aliwafungia wageni bao la kwanza dakika ya tatu. Niang aliifungia mabao dakika ya 10na 19, kabla ya bao la penalti alilofungwa dakika ya 68. Wenyeji walijipatia mabao yao kupitia kwa Patou Kabangu dakika ya 44 na 83.Cameroon wanaongoza Kundi E baada ya kuichapa Mauritius Jumamosi.Mechi ya Kund F, kati ya Gambia na Namibia mjini Banjul iliahirishwa, wakati Cedric Amissi aliipatia bao timu yake dakika tano na kuzifanya timu hizo za Kundi H, kati ya Burundi na Benin kumalizika kwa sare ya bao 1-1.Mabingwa wa Afrika, Misri ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Sierra Leone mjini Cairo.Pharaohs walipata bao lao kupitia kwa Alhassan Bangura dakika ya 56, lakini Mahmoud Fathallah aliisaiwazishia timu yake dakika nne baadaye.

Friday, September 3, 2010

JAMANI MSITULETEE SIASA KATIKA RIADHA.


Katibu mkuu wa chama cha soka cha riadha tanzania suleiman nyambui amesema kitendo cha agrey mareale kuambiwa kuwa sio mmiliki wa mashindano ya kilimanjaro marathon na walikuwa wakimtumia kama mshereshaji sio sahihi kabisa kwa (AT) kisa anatafuta umaarufu katika mambo mengine kitu ambacho suleiman nyambui amepinga kwani mbio hizo bila mareale sizingekuwapo

TWIGA STARS WAENDELEA NA MAZOEZI UWANJA WA KARUME



Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake wakiwa mazoezini

SERIKALI YATOA BARAKA KWA TIMU YA TAIFA YA NETIBALL

mwenyekiti wa baraza la michezo taifa idd kipingu akizumgumza na waandishi wa habari
Katibu mkuu wa bmt kushoto lihaya na mwenyekiti kipingu.

Serikali imeagiza timu ya netiboli ishiriki mashindano ya kimataifa kwa kuzingatia taratibu na kawaida ya muundo wa timu ya taifa uwepo wa wachezaji na viongozi wa zanzibar ni muhimu.

Hivyo serikali imekumbusha tena kuwa CHANETA NA CHANEZA kuafikiana katika uundaji wa timu ya taifa ili kudumisha muungano na tofauti zao zinatakiwa kumalizika mara baada ya kurudi katika mashindano hayo.

KUHUSU NGUMI ZA RIDHAA NA TENESI KIPINGU AMESEMA.

migomo inayotokea kwa wachezaji kugomea mashindano imetokana na uongozi mbovu ambao bado hajafahamu nini maana ya uongozi.

Amesema kwa upande wa ngumi viongozi na wachezaji wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali juu ya mgomo huo ,lakini baraza na wizara imegundua kuwa tatizo la mgomo huo ni viongozi jambo ambalo limetokea hata kwa mchezo wa tenesi hivyo katika kuondokana na matatizo hayo baraza la michezo taifa linatarajia kuandaa semina ya viongozi wa michezo mbalimbali kabla ya mwaka huu kuisha.