Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 16, 2012

BALOZI MPYA WA CHINA NCHINI TANZANIA AANZA KAZI, ATANGAZA VIPAUMBELE VYAKE ,AAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA TANZANIA NA CHINA

.

Balozi mpya wa China nchini Tanzania
Lu Youqing (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu awamu ya uongozi
wake nchini Tanzania na vipaumbele vyake katika kuimarisha ushirikiano na kuleta
maendeleo ya Tanzania na China leo jijini Dar es salaam. Wengine
kutoka kushoto ni Bw. Fu. Jijun mshauri wa masuala ya siasa katika ubalozi wa
china na Bw. HU Changming (kulia) ambaye ni mshauri mwandamizi wa uhusiano wa
ubalozi huo.
Waandishi wa habari kutoka katika
vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia hotuba ya balozi mpya wa
China nchini Tanzania Lu Youqing kuhusu awamu ya uongozi wake nchini Tanzania na
vipaumbele vyake katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China
Picha na Aron Msigwa
–MAELEZO.

Na. Aron Msigwa –
MAELEZO.
Dar es
salaam.
Balozi mpya wa
China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing amesema atahakikisha kuwa anatumia muda wa
uongozi wake kuwatumikia wananchi wa China na Tanzania na kuhakikisha kuwa
ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi katika nyanja za kiuchumi, kisiasa,
kiutamaduni na kijamii unadumishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za
ubalozi huo leo jijini Dar es salaam amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za
bara la Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kufuatia maendeleo na
mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanatokea duniani.

Amesema China ikiwa ni nchi ya pili
duniani kwa maendeleo itaendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali
katika bara la Afrika kuimarisha na kutetea amani, umoja, kushiriki katika
utatuzi wa migogoro mbalimbali inayotokea katika nchi za Afrika na
kusaidia nchi marafiki katika mipango ya maendeleo.

“Hivi sasa uchumi wetu unakua kwa
kasi sana na kufikia pato la taifa la dola za kimarekani trilioni 7.5 kwa mwaka
sawa na asilimia 9.2 maendeleo haya ni makubwa ” amesema.

Amefafanua kuwa maendeleo yaliyopo
nchini China kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na mfumo na sera nzuri
za uchumi zilizopo pamoja na mabadiliko ya wananchi kifikra na
kitabia na kuongeza kuwa kuna juhudi mbalimbali zilizofanywa katika kuinua
uchumi wa China zikiwemo utoaji wa huduma bora kwa wananchi, uzingatiaji wa
masuala ya ajira, matumizi ya sayansi na teknolojia na utoaji wa elimu bora kwa
wananchi.

Katika kuhakikisha kuwa ushirikiano
baina ya China na Tanzania unaendelezwa katika nyanja mbalimbali balozi Lu
amesema katika kipindi cha uongozi wake nchi yake itaendelea kuchangia kutoa
nafasi za ajira kupitia makampuni mbalimbali ya kichina na miradi mbalimbali inayoanzishwa nchiniTanzania katika sekta ya kilimo,
mawasiliano, utengenezaji wa miundombinu mbalimbali zikiwemo barabara, madaraja
na ujenzi wa mitandao ya mawasiliano.

“Kihistoria tuna ushirikiano mkubwa
sana baina ya Tanzania na China katika miradi
mbalimbali inayoanzishwa pamoja na miradi ya ushirikiano ya reli ya Tazara na
kiwanda cha Urafiki “ amesema Balozi Lu.

Ameongeza kuwa nchi yake itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika nyanja ya elimu katika utoaji wa
ufadhili na nafasi za masomo kwa watanzania kwenda nchini humo kujifunza masuala
mbalimbalina kuongeza kuwa nchi yake itaendelea kutoa
fursa kwa wasanii mbalimbali waliopo nchini kwenda China kujifunza
masuala mbalimbali ili kuboresha kazi zao na tasnia ya sanaa kwa
ujumla.

No comments :

Post a Comment