Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 9, 2012

MKALI WA FACEBOOK KUPIGA SHOO KESHO VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAM​A


Msanii
wa Mziki kutoka South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) kulia akizungumza na
waandishi wa habari, Dar es salaam jana kuhusu onesho lake la leo
litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kushoto ni Msanii
aliyeongozana nae Dumiseni Mkihanya.(Picha na www.burudan.blogspot.com)

Msanii
wa Mziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo A.K.A Ommy Dimpoz kushoto
akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuhusu Onesho lake
litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kulia ni msanii kutoka,
South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) na Dumiseni Mkihanya na Meneja wa
Kinywaji cha Savana, Diana Musheruzi.(Picha na
www.burudan.blogspot.com)


Na Mwandishi Wetu

CLEOPAS Monyepao
maarufu kama DJ Cleo mkali wa nyimbo ya Facebook kutoka Afrika Kusini kesho
anatarajia kutoa burudani katika viwanja vya Posta, Kijitintama Dar es
Salaam.

Dj Cleo ameambatana na wachezaji wake Dumisani Makihanya
'Bleksem' na Dj Soul T ambaye amekuwa akionekana katika video mbalimbali za
nyimbo zake.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Dj Cleo alisema amefurahishwa
sana na ujio wake hapa nchini ikiwa ni kwa mara ya kwanza na hiyo ni kutokana na
ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Alisema, anaamini
katika onesho lake hilo la kesho atajifunza mengi kutoka kwa Watanzania ikiwa ni
pamoja na kuwajua wanamuziki na muziki wa hapa nchini sambamba na Utamaduni kwa
kiasi fulani.

Aliongeza kuwa anahitaji sana kujifunza utamaduni wa
Tanzania kwani nchi hizo zinashirikiano mkubwa na zinaendana kwa mambo
mbalimbali kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na muonekano wa wananchi
wake.

Alisema, kwa upande wa burudani atawapa mashabiki burudani nzuri na
ambayo wataridhika nayo ingawa mashabiki wengi wanaujua wimbo wake wa Facebook
lakini yeye ananyimbo nyingi hivyo zitakuwa ni 'Supries' kwao.

"Watu
wengi wanaujua wimbo wangu wa Facebook lakini zipo nyimbo nyingi ambazo zitakuwa
ni mpya kwao na ninaamini watazipenda hivyo waje kwa wingi ili waweze kujionea
na kusikia," alisema.

Naye kwa upande wake mmoja wa wanamuziki ambao
wataimba jukwaa moja na DJ Cleo, Omari Nyembo 'Ommy Dimpoz' alisema, anajisikia
faraja kubwa kupanda jukwaa moja na msanii huyo kwani anaimani naye atajifunza
mengi kutoka kwa msanii.

Alisema, kupanda jukwaa moja na wasanii wa nje
kunawasaidia muziki wao kufahamika Kimataifa zaidi kwani utajulikana
ukilinganisha kazi yake hasa mwanamuziki huyo ni ya Udj.

Sambamba na
wanamuziki hao pia jukwaa hilo litapambwa na Suma lee, Dully Sykes, Juma Nature,
Tip Top Conection, Wanaume Halisi, Chege na Temba, Wanaume TMK na Wakali
Dancers

Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business
Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787
406938
+255774406938

- +255713406938

Po.Box. 15493
Dar es
Salaam Tanzania

No comments :

Post a Comment