Mkurugenzi wa
mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akiongea na
waandishi wa habari asubuhi hii katika hoteli ya Serena Dar es salaam wakati
alipotangaza udhamini wa kampuni hiyo katika maadhimisho ya wiki ya maji
yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa kuanzia Machi 16, katika picha wengine
kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Maeneja wa Mahusiano (SBL) na katikati Amani
Mafuru Naibu Mkurugenzi wa maji Vijijini.
mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akiongea na
waandishi wa habari asubuhi hii katika hoteli ya Serena Dar es salaam wakati
alipotangaza udhamini wa kampuni hiyo katika maadhimisho ya wiki ya maji
yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa kuanzia Machi 16, katika picha wengine
kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Maeneja wa Mahusiano (SBL) na katikati Amani
Mafuru Naibu Mkurugenzi wa maji Vijijini.
of Life” (WOL), ni mpango maalum
unaodhamiria kuwezesha upatikanaji wa maji safi ya kunywa na udhibiti wa usafi kwa watu wapatao milioni moja barani Afrika.
Maji yamepewa
kipaumbele katika biashara yetu kimataifa. Kampuni
ya Bia ya Serengeti imekuwa mstari wa mbele
kuhakikisha kuwa maji safi na salama pamoja
na usafi wa mazingira ni
jambo linalotiliwa mkazo.
Wiki ya maji ambayo itaanza tarehe 16 Machi itaadhimishwa siku ya Machi 22 mwaka
huu, ni jukwaa muhimu sana kutangaza na
kuweka msisitizo wa umuhimu wa utunzaj wa maji na vyanzo vyake.
Kwa kuiheshimu kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni “Maji
kwa usalama wa Chakula”,ni dhahiri kuwa
maji yanachukua nafasi kubwa sana na
hasa
katika ulizalishaji wa chakula na kilimo
kwa ujumla..
Tatizo la maji limekuwa likiathiri kila bara duniani na
zaidi ya asilimia 40 ya watu. Hadi kufikia mwaka 2025, watu bilioni 1.8 watakuwa
wanaishi katika nchi ama mikoa ambayo haina
maji safi kabisa, na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani inawezekana
wanaishi katika hali ngumu ya upatikanaji wa maji. Kukosekana kwa maji
kunawakosesha wakulima kuzalisha mazao ya kutosha kwa chakula na hata kujikimu
kimaisha.
Kampuni ya bia ya Serengeti mwaka huu imetenga zaidi ya
shilingi milioni mia tatu za kitanzania.
Milioni mia moja za kitanzania zikilenga
sherehe za maadhimisho mkoani Iringa kwa kudhamini vipeperushi, vijarida na
zaidi ya shilingi milioni mia mbili zikilenga kwenye miradi salama ya maji na
usafi katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dar Es Salaam na Iringa.
Tunasisitiza kuhusu swala la kuongezeka kwa changamoto
za tatizo la maji ulimwenguni, katika utendaji kazi wetu ndani ya kampuni na hata kwenye jamii inayotuzunguka.
Kama kampuni, Serengeti
(SBL), inafanya kazi kupunguza matumizi ya
maji katika vifaa vya uzalishaji na mfululizo wa utoaji wa bidhaa
zetu. Hii inahusisha uboreshaji madhubuti wa maji katika mitambo yetu, kuhakikisha kuwa matumizi ya maji katika
maeneo yetu yanazingatiwa, na kupunguza
majitaka (na nguvu ya maji hayo katika uchafuzi wa mazingira) kutoka kwenye mitambo
yetu.
Pia tumekusudia
kuongeza njia za upatikanaji wa maji kwenye jamii zinazotuzunguka na usimamizi
wa vyanzo vya maji.
Kama kampuni inayowajibika, kufanya
kazi na wengine kuendeleza lengo la Umoja wa Mataifa(UN) la Malengo ya
Milenia ya Maendeleo kwa ajili ya maji na
usafi wa mazingira na kupitia juhudi za
pamoja na wafanyakazi wetu, watumiaji, wateja, wagawaji, mashirika yasio ya
kiserikali, serikali, na biashara
nyingine tunafanya kazi kwa pamoja ili kuhamasisha na kutoa malengo yatakaotoa suluhisho la muda mrefu la kutatua shida ya maji
katika masoko yetu.
Programu hii ya
Water of Life(WOL), imekusudia kutoa
upatikanaji wa huduma ya maji safi, inaimarisha kazi
tunazofanya katika utendaji wetu wa
kazi. Tunatumia ujuzi, watu wanaotuzunguka washirika na wadau
wetu kuhakikisha kuwa maji safi yanapatikana hasa pale yahahitajika. Kwa Jamii, majumbani na kwa watu binafsi.
Biashara yetu imekuwa ikijihusisha na miradi mbali
mbali ya maji safi na mazingira kama
‘Mkuranga water project’ na moja nyingine ambayo ilikuwa ni
mradi ambao ulishirikisha makampuni na
mashirika yasio ya kiserikali ni mradi wa
uboreshaji wa huduma ya maji katika
hospitali ya Amana.
Kampuni ya Bia ya Serengeti na EABL foundation iliwekeza kiashi shilingi milioni 384.6 za kitanzania
katika mradi wa Mkuranga na zaidi ya watu 250,000 wamefaidika.
Tunatambua kwamba maji safi ni muhimu kwa maendeleo na
kwa kuchangia kuboresha afya ya jamii na
kiwango cha elimu na pia kupunguza umaskini. Mradi wa ‘Water Of Life
(WOL) ulizinduliwa na Diageo mwezi Juni mwaka 2006 kwa lengo la kutoa
maji safi ya kunywa kwa
walengwa. Diageo ilizindua mradi huu katika
nchi 14 nyingi zikiwa ni nchi za Afrika,
kwa kusadia miradi mbali mbali ikiwemo ya
uchimbaji wa visima, visima vya
mkono, uvunaji wa mvua, na mbinu
za kuchuja maji
Uwekezaji wetu katika jamii
utaendelea kwa kusaidia na kukamilisha kazi yetu katika utendaji wetu, ili
kupunguza athari za usambazaji wa maji taka na kuboresha upatikanaji wa maji safi ya kunywa katika mikoa
tunayofanya shughuli zetu.
No comments :
Post a Comment