Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, December 26, 2011

MSONDO YAFUNIKA TCC CHANG'OMBE USIKU WA KUAMKIA LEO










Mwanamuziki chipukizi mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya Msondo TX Moshi William TX Moshi William Hassani Moshi, TX,Junior, akinyanyuliwa juu juu na mashabiki wa bendi hiyo wakati alipokuwa akiimba katika mpambano wa bendi za Msondo Band na DDC Mlimani Park Sikinde jana, kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam.


Mpambano huo ulivuta mashabiki wengi katika viwanja vya TCC Sigara ambapo bendi ya Msondo, ilionekana kuwapiku wenzao wa Sikinde kutokana na Shamrashamra zilizokuwa zikitawala wakati Msondo wakiimba jukwaani, Onyesho hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo ikiwa ni pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismas.


Wanamuziki Shaban Dede na Hassani MoshiTX ,Junior wa Msondo wakiimba jukwaani huku mashabiki wakiwashangilia kwelikweli wakati wa onyesho hilo lililofanyika TCC Chang'ombe usiku wa kuamkia leo.


Hassani Moshi TX Junior akiimba katikati ya mashabiki , huku mashabiiki hao wakimshangilia.


Kutoka kulia ni mwimbaji wa Bendi ya Sikinde Hassan Kunyata, Yusuph Bernald na Shaban Lendi wapiga Saxaphone wakifanya vitu vyao jukwaani.


Mwimbaji wa bendi ya Sikinde Othman Kambi akicheza sambamba na wanenguaji wa bendi hiyo wakati bendi hiyo ilipotupa karata yake ya mwisho usiku wa kuamkia leo.


Mashabiki wakipanga mstari huku wakiserebuka na Msondo.


Umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria katika onyesho hilo usiku wa kuamkia leo.


Wadau wakijimwaga na muziki wa Msondo hebu wacheki.


Mpiga gitaa la solo wa bendi ya Msondo Said Mabela wa pili kutoka kushoto akila pozi kwa picha na wadau usiku wa kuamkia leo.

No comments :

Post a Comment