Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .
Siku kumi kabla ya mpambano mabondia Rashid Matumla na Maneno Osward walishauriana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu kama wanatumia na wameshapimwa na Daktari wa mchezo wa ngumi nchini Charles Kilaga, sheria za mchezo huo haziruhusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu
Hivyo mabondia wote wamekutwa wapo fiti na wanatarajia kuzipiga jumapili ya tarehe 25
Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'Mwayamwaya' ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawahi kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kushinda mara moja.inachukuliwa kwamba mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.
Mpambano huo Utasindikizwa na mabondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali. '' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja Mtagwa anayefanya shughuli zake Marekani. DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi, DVD hizo zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D.
No comments :
Post a Comment