Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, December 14, 2011

WANAFUNZI 567,567 WAFAULU MITIHANI YA DARASA LA SABA



Baadhi ya wanafunzi wakishangilia baada ya kumaliza Mtihani wa Darasa la Saba hivi karibuni.
Na Gradys Sigera na Magreth Kinabo – MAELEZO
JUMLA ya wanafunzi 567,567 wamefaulu mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011, na watafanyiwa mtihani wa majaribio kabla ya kuanza masomo yao rasmi katika shule walizochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Akitangaza matokeo hayo, jijini Dar es Salaam leo mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo (Mb.) amesema, utaratibu huo wa kufanyiwa majaribio utaanza mwakani 2012, ambapo wanafunzi waliofaulu watafanyiwa majaribio ya kupima stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Wakati huo huo, Baraza la Mtihani la Taifa limefuta matokeo yote ya watahiniwa 9,736 sawa na asilimia 1.0 waliobainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo.
“Mwanafunzi atakayebainika kuwa kajiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi hizo, Mwalimu Mkuu wa shule alikotokea mwanafunzi huyo na Msimamizi wa Mtihani wakumaliza elimu ya msingi watachukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Waziri Mulugo.
Akizungumzia kuhusu kiwango cha ufaulu alisema kimeongezeka hadi kufikia asilimia 58.28 ukilinganisha na cha mwaka jana ambacho kilikuwa asimilia 53.52.
Aliongeza kuwa kiwango cha ufaulu wa masomo ya Kiingereza, Sayansi na Hesabu kimepanda . Somo la Kiingereza kutoka asilimia 36.47 mwaka jana hadi asilimia 46.70 kwa mwaka huu , wakati somo la Sayansi ni asilimia 61.33 mwaka huu toka asilimia 56.05 mwaka jana na Hesabu asilimia 39.36 mwaka huu toka asilimia 24.70 mwaka jana.
Jumla ya wanafunzi 983, 545 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwezi wa Septemba 2011 na kuonesha kuwa, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 53.52 mwaka jana hadi 58.28. Jumla ya wasichana waliofaulu ni 27,377 na wavulana ni 289,190.
Wakati huo huo, Serikali imesema, kazi ya kuhakiki madai ya walimu imekamilika tangu Desemba 2, mwaka huu na kwamba madai hayo ni kiasi cha sh. bilioni 52.
Akijibu swali lililoulizwa na waandishi kuhusu madai ya walimu, Naibu Katibu Mkuu Bw. Selestine Gesimba amesema, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 30 ni za mishahara na bilioni 22 ni za madai mengineyo.

Bw. Gesimba ameongeza kuwa, madai ya malipo mengine yataanza kulipwa mwezi huu (Desemba) na madai ya malipo ya mishahara yatalipwa ifikapo Januari 2012.

Hata hivyo alisema tayari Hazina wameshalipa bilioni 28 za madai ya mishahara kuanzia Julai mwaka jana hadi Novemba mwaka huu.
Naye Francis Godwin wa Iringa, anaripoti
MKOA wa Iringa umeendelea kupiga hatua katika ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba baada ya watahiniwa 47979 waliofanya mtihani huo wanafunzi 33409 sawa na silimia 69.9 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo mwaka huu kufaulu .

Pamoja na ufaulu huo jumla ya wanafunzi 737 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefutiwa matokeo yao kutokana na kufanya udanganyifu katika ufanyaji wa mitihani hiyo.

Kutokana na hali hiyo Serikali mkoani Iringa imezipongeza Halmashauri za wilaya ya Kilolo na Iringa vijijini kwa kufanikisha kupiga hatua katika ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba .

Mwenyekiti wa kikao cha uteuzi wa wanafunzi waliofaulu mkoa wa Iringa katibu tawala wa mkoa Getrude Mpaka alisema kuwa ufaulu wa wanafunzi hao ni changamoto kubwa kwa wilaya kuongeza
idadi ya vyumba vya madarasa pamoja na kuongeza madawati zaidi.

No comments :

Post a Comment