Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, December 13, 2011

FID Q, ROMA WAFUNIKA TAMASHA LA TIGO





Wanamuziki wa kundi la Tip Top Connection la jijini Dar es Salaam wakitoa burudani katika tamasha maalum la kusherehekea miaka 50 ya Uhuru liloandaliwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo katika Ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam juzi.


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Godzila akitoa burudani katika tamasha maalum la kusherehekea miaka 50 ya Uhuru liloandaliwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo katika Ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam juzi.


Mwanamuziki Twenty Percent akitoa burudani katika tamasha maalum la kusherehekea miaka 50 ya Uhuru liloandaliwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo katika Ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam juzi.

---

Na mwandishi wetu

Wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Roma Mkatoliki pamoja na Fid Q juzi walitoa burudani yenye mvuto zaidi katika tamasha maalum la kusherehekea miaka 50 ya Uhuru lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Wanamuziki hao walizikonga nyoyo za umati mkubwa wa watu uliohudhuria katika tamasha hilo, kwa umati huo kuimba kwa kuwafuatisha wanamuziki hao ambao walipanda jukwaani kutoa burudani kwa nyakati tofauti .

Mbali na wanamuziki hao kutoa burudani iliyoonekana kuvuta hisi za watizamaji waliofika katika tamasha hilo, wanamuziki wengine waliotoa burudani katika tamasha hilo ni kundi la Tip Top Connection, Twenty Percent, Godzilla na wasanii wengine wanaochipukia katika muziki wa Kizazi kipya.

Tamasha hili ambalo lilifanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo, jumamosi na jumapili liliandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, ikiwa na lengo la kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, kama sehemu ya kutoa shukrani kwa wateja wake.

Akiongea wakati wa Tamasha hilo mwakilishi wa Tigo Benny Lutaba alisema kuwa Tamasha hilo liliwaopa nafasi pia wateja wa Tigo kupata bidhaa mbalimbali pamoja na huduma nyingine za Tigo kwa bei nafuu. “ Siku hizi mbili wateja wetu wamepata burudani ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru na pia kupata fursa ya kujipatia huduma zetu kwa bei nafuu,” alisema.


No comments :

Post a Comment