Mwisho wa mwaka 2011 utaleta furaha mpya na matumaini kwa vijiji 6 kufuatia makabidhiano ya visima 6 katika maeneo mbalimbali yenye uhaba wa maji katika kanda ya Bagamoyo kupitia mradi wa Walk for Water-mpango wa Spearhead Africa Limited. Visima 6 ni msaada kutoka Belgian Technical Co-operation, Tanzania Distillers Limited na mradi wa Walk for Water.
Baada ya miezi 8 mfululizo ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali kukamilisha lengo la mradi wa Walk for Water 2011, sasa mradi huu umefikia hatua za mwisho katika ujenzi wa visima 6 katika maeneo tofauti yenye uhaba wa maji katika ukanda wa Bagamoyo. Lengo la mpango kwa mwaka 2011 ni kujenga uelewa wa uhaba wa maji kimataifa na ndani ya nchi na kujenga visima na kupata vituo vya upatikanaji maji katika vijiji vya Bagamoyo kwa msaada wa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi.
Mpango huu unaonyesha nguvu ya ushirikiano wa sekta ya umma binafsi katika kubadili maisha ya baadhi ya watanzania wenye matatizo mbalimbali na kwa juhudi ya pamoja kutoa baadhi ya huduma za msingi kwa jamii. Kwa lengo la kuleta mabadiliko kwa watu wenye bahati ya chini, visima hivi vitasaidia wakazi wa Bagamoyo katika kupata maji safi na salama si tu kwa ajili ya shughuli zao za kila siku lakini pia katika kudumisha afya na masuala ya usafi wa mazingira katika vijiji.
Kufanya kazi kwa kushirikiana na ofisi ya Manispaa ya Bagamoyo, Ifakara Health Institute-waanzilishi wenza wa mradi wa Walk For Water 2011, imeanzisha Kamati za Maji katika kila kijiji kwenye vijiji vyote 6. Kamati imeundwa kwa ajili ya matengenezo endelevu ya kisima. Wanachama wa Kamati ya Maji watapewa kitabu na mafunzo yanayohitajika kutoka kwa wenza wetu Ifakara Health Institute juu ya kudumisha kisima na itakuwa na wajibu wa kuhakikisha matumizi sahihi ya maji ya wanakijiji.
Wakati wa uzinduzi wa moja ya visima, bi. Bertha Ikua-Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Spearhead Africa Limited alisema “Tungependa kutoa shukrani zetu kwa Tanzania Distillers Limited na Belgian Development Co-operation na wote walioshiriki katika tukio la Walk for Water na kudhamini visima vilivyojengwa chini ya mradi wa Walk for water. Tungependa pia kuwashukuru Dr Salim Abdulla-Mkurugenzi wa Ifakara Health Institute na Mr. Peter Sasse kwa kushirikiana nasi katika juhudi hii-muda wao wa thamani na kujitolea kwao sio tu unashukuriwa na sisi, bali pia na wanawake na watoto wa kijiji hiki”. “Shukrani zetu zimuendee Bi Margaret Masanga-katibu wa mbunge Ofisi ya Manispaa ya Bagamoyo kwa muda wake na kujitolea kwa kutoa msaada katika kutambua maeneo muhimu ambayo yana haja ya maji, pia, kwa kusaidia upatikanaji wa vibali na nyaraka na kurasimisha kisima pamoja na manispaa na kamati na kwa msaada wao mkubwa katika mradi huo.” Uchimbaji wa visima hivi 6 ni ushahidi tosha wa kauli mbiu ya mradi wa Walk for Water:Kila hatua ina thamani. Kila tone lina thamani.Kila mchango una thamani. Mpango huu unahamasisha wabia wengine kujiunga na miradi kama hii ili kuleta tofauti katika maeneo yenye mahitaji.
No comments :
Post a Comment