Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa Kariakoo Kota za Bandari kata ya Gerezani wameitaka serikali kutowahamisha wala kuwavunjia nyumba zao hadi hapo kesi yao iliyopo mahakama kuu kitengo cha Ardhi itakapo kamilika.
Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa mtaa huo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuwa nyumba hizo walinunua kutoka serikali na kupewa mkataba.
Alisema eneo hilo linataka kuchukuliwa na serikali ili kujenga kituo cha mabasi yaendayo kasi bila ya kujali kuwa nyumba hizo waliuziwa ambapo serikali iliingia mkataba na mtu mmoja mmoja.
"Tumesikia fununu kuwa serikali inataka kuja kuvunja nyumba zetu kinguvu ikiwa kesi bado ipo mahakamani",alisema
Kwa upande wake katibu mwenezi wa siasa wa chama cha Mapinduzi Bw.Akida Hafidhi alisema serikali ilifanya makosa kuingia katika eneo hilo ikiwa inajua kabisa kuna mgogoro na kuongeza kuwa wanaomba haki iweze kutendeka kwa kuiachia mahakama kutoa maamuzi kama katiba inavyoelekeza.
Alisema serikali inatakiwa kutambua kuwa wakazi wa eneo hilo wanamiliki nyumba hizo kimkataba na hakuna mtu aliyevunja mkataba huo ambapo walinunua kutoka kwao.
Hata hivyo walisema watashangazwa endapo watasikia kuwa kuna mtu anaingilia uhuru wa mahakama ikiwa ibara ya 4(1) na 107(a) ya katiba ya Tanzania inaeleza wazi kuwa chombo cha mwisho chenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ni mahakama ya Tanzania.
"Tumesema hivyo kwa sababu tulisikia baadhi ya watendaji serikalini walisema tulienda mahakamani kimakosa huku wakijua dhahili kuwa ni mahala ambapo haki inapatika",walisema
Walisema wanamuomba Rais Jakaya Kiwete asije akadanganywa kwa hilo kuwa kuna makubaliano yaliofanyika huku wakisisitiza kuwa kesi iliyopo ni kuvunjwa kwa mkataba na sio madai ya fidia kama ambavyo baadhi wa watendaji walivyopeleka taarifa serikalini.
No comments :
Post a Comment