|
Baadhi ya
viongozi wa TAWA akiwemo Katibu Mkuu Magnus Simon (aliyeshika dambeli)
wakiwa na baadhi ya wachezaji katika ukumbi wa Mayfair Plaza |
|
Baadhi ya viongozi wa TAWA wakiwa na wachezaji wa mchezo huo wa kunyanyua vitu vizito |
|
Rais wa
Shirikisho la Wanyanyua Vitru Vizito Mr Kyler toka Marekani ( wa pili
toka kulia) akiwa na baadhi ya wachezaji wa Tanzania alipotembelea hapa
nchini hivi karibuni. |
|
Wachezaji wa timu ya taifa wa mchezo huo wakionyesha umwamba mbele ya viongozi wa TAWA |
|
Tupo fiti kinoma...tupelekeni Botswana tukalete medali |
|
Titus Joseph akijiandaa kunyanyua chuma mbele ya wenzake |
|
Katibu Msaidizi
wa TAWA, Hillary Kahinji (wa kwanza kushoto mbele) akifanya mazoezi na
wachezaji wa timu ya mchezo huo kwenye ukumbi wa Mayfair Plaza |
|
Mkurugenzi wa
Idara ya Michezo nchini, Leonard Thadeo ( wa pili toka kushoto) akiwa na
viongozi wa TAWA mara baada ya kuchaguana mwezi uliopita. |
CHAMA cha Wanyanyua Vitu Vizito Tanzania (TAWA) kimeandaa hafla maalum
itakayotumika kuendesha harambee ya kusaka fedha za kuiwezesha Timu ya
Taifa ya mchezo huo kwa Vijana kwenda kwenye michuano ya Afrika
itakayofanyika nchini Botswana mwezi ujao.
Katibu Mkuu wa TAWA,
Magnus Simon, aliiambia MICHARAZO kuwa, hafla itakayoambatana na
uzinduzi wa chama hicho kilichofufuliwa upya itafanyika siku ya Mei 3
mwaka huu kwenye ukumbi wa Mikocheni Resort, ambapo wanatarajiwa wageni
mbalimbali na wadau wa mchezo huo watahudhuria.
Simon alisema
wamekusudia kukusanya si chini ya Sh. Milioni 20 zinazoweza kuwasaidia
kupeleka kikosi cha wachezaji watano katika michuano hiyo ya Vijana ya
Afrika itakayofanyika Botswana kati ya Mei 22-26.
"Baada ya kukwama
kutuma timu katika michuano ya Afrika kuwania kucheza michezo ya Olmpiki
kwa vijana nchini Cameroon, tunapigana angalau tuweze kutuma timu
Botswana na tumeandaa hafla itakayoambatana na harambee ya kuchangisha
fedha kwa ajili ya jambo hilo," alisema Simon.
Simon, alisema hafla
hiyo mbali na kuendeshwa kwa harambee pia itapambwa na mazoezi na
shindano ndogo la wanyanyua vitu vizito na wale ambao watafanya vyema
watazawadiwa pamoja na kuongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa,
kinachoendelea kujifua kwenye ukumbi wa Mayfair Plaza.
Katibu alisema
wachezaji hao wa taifa ndiyo pia watakaokuwa sehemu ya
watakaoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa baadaye nchini
China na Uganda.
Simon alisema mpaka sasa TAWA imefanikiwa kupata
wadhamini wachache ambao ni Akbar Jaffer wa Mayfair Plaza, Mikocheni
Resort Centre (MRC), Saada Beauty Para na blogu hii (MICHARAZO
MITUPU)ambao wamekuwa bega kwa bega na uongozi waop katika kukirejesha
chama chao katika uhai baada ya kuwa kimya kwa miaka 9 na kuwaomba
wengine wajitokeze kwa ajili ya kufanikisha hafla hiyo ya Mei 3.
"Tunayaomba
makampuni, asasi na watu binafsi watusaidie tufanikishe hili, ili
Tanzania tukashiriki michuano hiyo na kurejesha heshima katika anga la
kimataifa baada ye soka na michezo mingine kukwama kusuuza nyoyo za
mashabiki," alisema Simon.
No comments :
Post a Comment