Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, April 16, 2014

DAR MORDEN TAARAB




Na Andrew Chale
KUNDI la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan Safaa  (Malindi),  wanatarajiwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wa burudani wakiwemo mashabiki wa soka wa Azam Fc waliokwisha chukua ubingwa  Ligi kuu Tanzania Bara,  kwenye onyesho maalumu la ‘Usiku wa Mwambao Asilia’, ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam, Aprili 19.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mratibu wa onyesho hilo la pamoja Dar Modern na Nadd Ikhwan Safaa   (Malindi ya Zanzibar), Bakari Hassan alisema hilo la Usiku wa Mwambao Asilia, litaenda sambamba na kuwapongeza mashabiki wa soka wa Azam Fc waliotwaa ubingwa huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza 2013/2014.

“Usiku wa Mwambao asilia, Aprili 19, pale Travertine utakuwa na shamrashamra mbali mbali ikiwemo za kuwapongeza Azam na mashabiki wao watakaofika kwenye onyesho hilo maalum” alisema Bakari.

Kwa upande wake, Mlezi wa Heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema usiku huo pia utakuwa ni maalum  ikiwemo pia kuwakutanisha magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, ambao wataimba nyimbo za zamani na za sasa.

“Kwa kiingilio cha sh 10,000 tu, usiku huo utapambwa na ‘surprise’, mbalimbali kwa wadau kupita kwenye zuria jekundu ‘red carpet’ na kupiga picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria usiku huo” alisema Asia Idarous.

Aidha, Asia, alisema tayari tiketi za onyesho hilo zimeshaanza kuuzwa sehemu mbalimbali ikiwemo duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda. Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions nawww.nakshi255.com

No comments :

Post a Comment