Makamu
mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino
Ramadhani akiongea jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa
mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee,
Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The Open Society
Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA). Kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina, pamoja na Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba.
Kamishana
wa zamani wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar - ZEC, Dkt. Nassor Seif
Amour akitoa ufafanuzi jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika
wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya
kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The Open
Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA). Pembeni ni
Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu
Augustino Ramadhani na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi
vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya,
wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya
ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya
The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA).
Washiriki
walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na
katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya
kiserikali ya The Open Society Initiative For Eastern African
Tanzania (OSIEA).
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi
vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya,
wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya
ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya
The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA).
Washiriki
walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na
katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya
kiserikali ya The Open Society Initiative For Eastern African
Tanzania (OSIEA).
Washiriki
walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na
katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya
kiserikali ya The Open Society Initiative For Eastern African
Tanzania (OSIEA).
Mkurugenzi
wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHWashiriki walioshiriki
katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya
kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The Open
Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA).
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo.
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akiuliza swali mara baada ya majadiliano.
Katibu
Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akijadili jambo na Mkurugenzi wa
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba
(kushoto) na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina (kati).
Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Aliyekuwa
makamu mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Mstaafu
Augustino Ramadhani amewataka wajumbe wa bunge maalumu la katiba
kujadili vipengele vya rasimu hiyo kwa kuviboresha badala ya kulumbana.
Jaji
Ramadhani ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mjadala
kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala
ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya OSIEA.
Amesema
kuwa, tume ya mabadiliko ya katiba imefanyakazi yake ya kuwasikiliza
wananchi na kuandika rasimu ambayo ipo mbele ya wajumbe hao, na hivyo
kutoa wito kwao kujadili kwa makuni ili kutengeneza mustakabali mzuri wa
Tanzania kwa kuzingatia hoja na kila upande wa Muungano.
“Sisi
kama tume tumefanya kwa kadiri ya uwezo wetu na tumepata rasimu ya pili,
sasa ni jukumu la wajumbe wa bunge la katiba kujadili na kuboresha
vipengele vilivyomo kwenye rasimu hiyo na kuachana na malumbano”.
Alisema Jaji Ramadhani.
“kila
mmoja akitaka kipengele chake kiwemo kwenye rasimu hiyo, ni jambo
lisilowezekana, kinachotakiwa hapa ni wajumbe kujadili na kupendekeza
mambo yenye maslahi kwa taifa kwa sasa na baadae”. Alisisitiza Jaji
Ramadhani
Jaji
Ramadhni amesema, vipengele vinavyobishaniwa vinajadilika na vinaweza
kuboreshwa zaidi kwa malahi ya pande zote mbili ili kupata katiba yenye
kutoa nafasi kwa kila upande wa Muungano katika kushiriki katika ujenzi
wa taifa.
“Vipengele
vinavyoshindaniwa vinafaamika na wajumbe wanaweza kutumia busara
kuvijadili na kuvitolea maamuzi kwa manufaa ya nchi ambayo inasubiri kwa
hamu Katiba Mpya” alisema Jaji Ramadhani.
Akiongelea
nafasi ya vyombo vya habari kwenye mchakto huo Muhadhiri wa Chuo Kikuu
cha Dar es salaam Dr Ayoub Rioba amesema, bado vyombo vya habari
havijapewa nafasi ya kutosha kisheria kushiriki katika kuelimisha umma
kuhusiana na mchakato huo.
“
Vyombo vya habari bado havijapewa nafasi yoyote kwenye mchakato huu bali
vinafanya kazi kwa mazoea na pia kuna vipingamizi vingi vinawekwa
kuwazuia waandishi wa habri kuandika habari za bunge la katiba” alisema
Dr Rioba.
Kamishana
wa zamani wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar –ZEC, Dr Nassor Seif Amour
amwataka wajumbe wa Bunge la katiba kuzingatia matakwa ya wananchi
badala ya kujadili maoni yao binafsi ama matakwa ya vyama
wanavyoviwakilisha.
“Sisi
tunawakumbusha wajumbe wa bunge maalumu la katiba kukumbuka maoni
wanayoyajidili kuwa ni ya wananchi sasa wasiweke maoni yao ama ya chama
katika mchakato huu ili wasitunge rasimu mpya badala ya kuiboresha”.
Alisema Dr. Nassor.
Mjadala huo umehudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi, asasi za kiraia na wanasiasa.
No comments :
Post a Comment