Picha haihusiani na habari, ila watoto wakifurahia kuoga kwenye bwawa la kuogolea kama wanavyuoonekana |
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum Suleiman Kova amefafanua juu ya taarifa ya vifo vya watoto watatu
waliofariki wakati wakiongolea kwenye bwawa la hoteli.
Kamanda Kova alisema April
27 kulitokea vifo vya watoto 3 ambao walikua na birthday party
nyumbani lakini baada ya kukamilika kwa taratibu za party ya nyumbani
waliamua kuimalizia party hiyo hotel ya Landmark,walipofika walienda
kuogelea kwenye swimming pool ya watoto lakini baadae watoto hao
walitoka kwenye pool ile ya watoto wakaingia kwenye pool ya wakubwa na
kwa bahati mbaya waliingia sehemu yenye kina kirefu.
Watoto wenzao walipoona wenzao wanazama walianza kuwavuta kuwatoa nje
lakini hali zao tayari zilikua mbaya, mmoja wapo hali yake ilikua kidogo
afadhari lakini kwa bahati mbaya nayeye alifia hospital wakati
akipatiwa matibabu katika hospitali ya Masana na kufanya Idadi ya watoto
waliofariki kuwa 3 majina yao ni Janet Zacharia, Eva na Ndimbuni.
Kamanda Kova amesema; "’Kusema kweli sio mara ya kwanza
kutokea, mara nyingi vifo vya watoto vinatokana na uangalifu au uzembe
kutoka kwa wale wanaotakiwa kuwaangalia hao watoto wao, hizi hotel zote
zenye swimming pool lile eneo la kuogelewa basi wasiruhusiwe watoto
wadogo kuogelea au kuwe na mtu ambaye anajua kuogelea au kuokoa ambaye
yupo pale’
‘Unajua watoto wana tabia ya kuigana mmoja akiingia akiogelea pengine
anafahamu kidogo wengine wote wanafata mkumbo wanaona wanaweza,sisi
kama jeshi la Polisi tumeamua hili kosa la uzembe kusababaisha kifo
kisheria mtu anaweza kushtakiwa kwa kuzembea kwa kutochukua tahadhari
mpaka watoto kama wale ambao hawana hatia uwezo wao mdogo wa kufikiri au
kuijiokoa’
‘Tunafatilia kwa umakini lakini jukumu la kufatilia maisha ya watoto
ni la wazazi mia kwa mia wasipofanya hivi wakiwa hawapo makini matokeo
yake ni haya watoto 3 wamefariki,tunaendelea na uchunguzi na baadae
tutatoa taarifa kamili’.
No comments :
Post a Comment