Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza
Hatimaye
Kikosi Kazi cha Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ndio waratibu
na waandaaji wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania
yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents (TMT) kinaondoka leo asubuhi
Mkoani Mwanza Kuelekea Mkoani Dodoma kwaajili ya kuendelea na shindano
la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Kati ambapo mashindano
yatafanyika Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa African Dream kuanzia
Jumamosi ya tarehe 12 April 2014 kuanzia Saa moja asubuhi hadi tarehe 15
April 2014, kabla ya mashindano hayo kufanyika Mkoani Dodoma mnamo Siku
ya Ijumaa tarehe 11 April 2014 kutakuwa na Promo pati itakayofanyika
katika Ukumbi wa Disco wa 84 Mjini Dodoma na Wasanii Lulu, Joti, Rich
Rich, Monalisa na MC Pilipili watakuwepo ndani ya nyumba.
Mashindano
haya yatakuwa ni muendelezo wa mshindano yaliyoanza kufanyika katika
Kanda ya ziwa Mkoani Mwanza ambapo Washindi watatu kutoka Mkoani Mwanza
wakiwakilisha Kanda ya Ziwa wakiwa wameshapatikana na kila mshindi
aliweza kupewa zawadi ya shilingi laki tano kila mmoja na kusubiria
kwenda Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kuungana na washindi wengine Wa
kanda zilizobaki kwaajili ya Fainali kubwa itakayofanyika mkoani Dar Es
Salaam na mshindi katika Fainali hizo ataibuka na Kitita cha Shilingi
Milioni 50 za Kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya
Proin Promotions Limited na washindi kumi bora watakaopatikana katika
Fainali hiyo watacheza filamu ya kwao na hatimaye itauzwa Nchini Nzima.
Katika
Mashindano haya ya Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania yajulikanayo kama
Tanzania Movie Talents yatajumuisha kanda ya Juu Kusini ambapo
yatafanyika Mkoani Mbeya, Kanda ya Kaskazini ambapo usaili utafanyika
Mkoani Arusha, Kanda ya Kati zoezi litafanyika Mkoani Dodoma, Kanda ya
Kusini ambapoo usaili utafanyika Mkoani Mtwara, Kanda ya Pwani ambapo
usaili utafanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mashindano haya
yakapewa upendeleo tena kufanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Kigoma Kwa
kuelewa kuwa Kigoma ni Mkoa ambao una wasanii wengi wa muziki wa bongo
fleva na Proin Promotions Limited kutoa nafasi ya Upendelo kwa kuhisi
pia wanaweza kupata Vipaji vya uigizaji Tanzania katika Mkoa Huo.
Mshindi katika Fainali ya mwisho ataibuka na Shilingi Milioni 50 za
kitanzania.
Katika
Mashindano haya Fomu zitapatikana siku ya Usaili na hakuna gharama
zozote zile zitakazotozwa kwaajili ya usaili na tunawaomba Wakazi wa
Kanda ya kati kujitokeza kwa wingi Mkoani Dodoma siku ya usaili na
kuweza kuonyesha vipaji vyao maana hii ndio fursa pekee ambayo
watanzania wanaipata kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na
hatimaye kuweza kutimiza ndoto zao za kuwa waigizaji katika tasnia ya
filamu nchini .
Shindano hili la Tanzania Movie Talents lina lengo la kusaka na kuibua Vipaji vya kuigiza na kukuza tasnia ya filamu nchini.
No comments :
Post a Comment