Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tff Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela amesema kutokana na kamati ya nidhamu iliyokaa jana na kupitia masuala mbalimbali yahusuyo ligi hiyo hivyo kuamua kutoa adhabu kwa wachezaji,vilabu na waamuzi ili kuhakikisha soka la Tanzania linakua.
Kutokana na adhabu hiyo Kiungo huyo kwa sasa ataendelea na adhabu zote mbili ikiwa ile ya kwanza alipewa adhabu kama hiyo katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya African Lyon uliochezwa kwenye dimba la Uhuru Agasti 23 ambapo mpaka sasa ameshatumikia siku 7.
Mbali na adhabu hiyo klabu ya Maji Maji pia imetakiwa kutoa kiasi cha shilingi laki 5 kutokana na mashabiki wake kuonyesha utovu wa nidhamu.
Mwakalebela ameongeza kuwa kamati hiyo pia imewaondoa baadhi Waamuzi katika orodha kutokana na kushindwa kumudu katika kuendesha michezo yao kitu kilichopelekea kupata alama chache walizopewa na makamisaa wao.
Baadhi ya Waamuzi hao ni Peter Mujaya aliyeshindwa kuchezesha mchezo kati ya Simba na Toto African uliochezwa Septemba 5 mwaka huu wakati Athuman Lazi naye ameondolea katika orodha hiyo baada ya kushindwa kumudu mpambano kati ya Azam fc na Moro United uliopigwa Septemba 9.
Hata hivyo waamuzi wote waliochezesha mchezo kati ya Maji Maji na Mtibwa Sukari mchezo uliochezwa Septemba 9 mwaka huu nao wameondolewa katika orodha hiyo ambao ni Othaman Kazi,Omar Miyaya,Omar Mfaume na Kamwanga Tambwe.
No comments :
Post a Comment