
Kiungo wa kimataifa wa Kenya Macdonald Mariga anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na matajiri wapya wa England Manchester City akijiunga na klabu hiyo akitoa klabu ya Parma FC ya Italia.
Mariga atakuwa mchezaji wa kwanza toka Kenya kufanikiwa kucheza katika ligi kuu ya England.
Manchester City imeripotiwa kukamilisha taratibu zote na klabu ya Parma kwa ajili ya kumnunua kiungo McDonald Mariga aliyetokea kutamba na klabu hiyo kongwe nchini Italia.

Kiungo huyo mkabaji amekuwa akizidi kuwa bora kila siku na amekuwa akiwindwa na klabu mbali kwa mida mrefu sasa ikiwa ni pamoja na Arsenal na Inter Milan.
Lakini kocha wa Manchester City Roberto Macini sasa ameripotiwa kufanikiwa kuwashawisho matajiri wa klabu hiyo kumnunua kwa dau la Pauni milioni saba.
Mama yake Mariga Mildred Wanyama ameripotiwa nchini akisema anamuombea mwanawe afanikiwe hilo.

Hata hivyo kufuatia Kenya kuwa nafasi ya 98 kiungo huyo mkabaji ameshindwa kupata kibali cha kufanya nchini England, hivyo dili kama kuingia mchanga vile.
klabu ya Inter Milan sasa itakuwa nanafasi kubwa ya kumnyakua.
No comments :
Post a Comment