(NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO)
DAR ES SALAAM
Chama
cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania
(TEWUTA) kimeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TICRA), kupunguza
tozo inayolipwa na makampuni ya simu nchini.
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dare s Salaam leo, Katibu Mkuu wa chama
hicho Junus Ndaro amesema TCRA imeshindwa kusimamia na kuhakikisha
gharama za huduma za mawasiliano ya simu zinapungua na kuwa na uwiano
sawa kwa tozo za makampuni yote Tanzania.
“Mamlaka
imeshindwa kuwaeleza watanzania kwa uwazi na huku ikitambua kuwa moja
ya jukumu lake ni kupanga bei elekezi kwa makampuni ya simu, kitendo
ambacho hakijafanyika toka mamlaka hiyo iundwe na kutangazwa kwenye
vyombo vya habari”, amesema Ndaro.
Ameongeza
kuwa pamoja na mambo mengine chombo hiki kiliundwa kwa madhumuni ya
kumsaidia mteja kupata bei nafuu kila anapotumia mtandao wowote wa simu.
“Ni
ukweli kuwa watanzania wamechoka kutembea na simu zaidi ya moja za
mitandao tofauti kwa sababu ya kutafuta punguzo kwa mtandao husika,
hivyo ni wajibu wa TCRA kusimamia mitandao yote ya simu nchini kuwa na
bei zenye uwiano wa karibu” amesisitiza Ndaro.
Ndaro
amesema kuwa serikali imeleta Mtandao wa Mkongo (FIBRE) ambao gharama
zake za uendeshaji ni mdogo sana na unafanya kazi vizuri kwa haraka
zaidi hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa TCRA kupunguza gharama wanazotoza
kutoka kwenye makampuni ya simu.
No comments :
Post a Comment