Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Moro United lililochezwa jana
(Aprili 23 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
28,688,000.
Jumla
ya watazamaji 7,945 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio
vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 6,946
kati ya hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada
ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,376,135.59 kila klabu ilipata
sh. 4,919,009.32, uwanja sh. 1,454,286.44.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 1,454,286.44, Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,058,414.58, Mfuko wa Maendeleo
ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 727,143.22, Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
sh. 145,428.64 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 1,454,286.44.
Gharama
za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli
ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000, mwamuzi wa akiba sh.
30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 80,000, gharama ya
tiketi sh. 3,000,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme
sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina
(Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Nayo
mechi kati ya Villa Squad na African Lyon iliyochezwa Aprili 22 mwaka
huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam iliingiza sh. 496,000 ambapo
kila klabu ilipata sh. 68,061.70 wakati watazamaji walioshuhudia mechi
hiyo ni 469.
No comments :
Post a Comment